IDARA YA UJENZI
Idara ya ujenzi ni mojawapo ya idara kuu zinazounda Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Lengo kuu ni kusimamia ujenzi wa majengo ya Serikali na kutoa ushauri wa namna iliyobora ya ujenzi huo;
Pia miradi ya Mashirika yasiyo ya ki – Serikali pamoja na kutoa ushauri wa ujenzi wa nyumba bora kwa wananchi , Kusimamia matengenezo ya magari, mitambo na nishati ya umeme kwenye majengo ya Serikali katika Halmashauri ya Wilaya.
Idara ya Ujenzi husimamia ukarabati naujenzi wa majengo mbalimbali katika Halmashauri yaWilaya ya Kiteto kama ifuatavyo:
Pia idara hutoa ushauri wa namna iliyobora ya ujenzi wa majengo katika miradi ya Mashirika yasiyo ya ki – Serikali pamoja na kutoa ushauri wa ujenzi wa nyumba bora kwa wananchi.
UMEME
Idara ya ujenzi pia kuna kitengo cha umeme. Kitengo hiki kupitia mtaalamu wetu wa idara hufanya shughuli za ukarabati nauwekaji wa mfumo wa umeme katika majengo yote ya halmashauri na serikali yaliyopo hapa wilayani.
MAGARI NA MITAMBO.
Idara ya ujenzi huyafanyia matengenezo madogomadogo magari na mitambo ya serikali katika karakana yake, pia huratibu na kukagua magari yote ya Halmashauri kwa ajili ya matengenezo mbalimbali kupitia mtaalamu wa magari wa Idara. Magari yote ya Halmashauri hukaguliwa kwanza na mtaalamu wa magari wa idara kabla ya kupelekwa kwa wazabuni kwa ajili ya matengenezo makubwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa