• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wilaya ya Kiteto Yang’ara Ufaulu Darasa la Saba 2018

Imetumwa : October 29th, 2018

Afisa elimu msingi ( W) Ndg. Emmanuel Mwagala akizungumza kuhusu matokeo ya darasa la saba ofisini kwake mapema leo.


HABARI KAMILI


Afisa Elimu msingi wilaya ya Kiteto ndugu Emmanuel Mwagala amewapongeza walimu wa shule za msingi wilayani hapa kwa jitihada walizozifanya katika ufundishaji ,ambapo kupitia jitihada hizo , katika matokeo ya mitihani ya darasa la saba mwaka 2018 kiwango cha ufaulu kimeongezeka.Mwagala ameyasema hayo katika mahojiano mafupi yaliyofanyika ofisini kwake mapema leo.

Akizungumza wakati wa mahojiano hayo Mwagala amesema “Matokeo ni mazuri sana yametutia moyo,walimu wamefanya kazi . Pamoja na mazingira magumu , lakini tumeweza kupata ufaulu wa asilimia 69.5, kwa wilaya kama hii yenye changamoto nyingi,huo ni ufaulu mzuri,lakini pia lengo letu ni kufanya vizuri zaidi, na tunaamini kwamba hilo linawezekana”.

Mwagala amefafanua zaidi kuhusu kiwango hicho cha ufaulu hapa anasema “Jambo lingine ambalo limetufurahisha ni kwamba wilaya yetu imetoa shule bora, katika shule ambazo zina watahiniwa zaidi ya 40,shule ya msingi  Boma imekuwa ya kwanza kimkoa , si hivyo tu bali katika kundi hilo la shule zenye watahiniwa zaidi ya 40 shule hiyo  imeshika nafasi 54 kitaifa jambo ambalo ni la kujivunia sana”.


Kadhakika Mwagala amesema kwamba kuna mabadiliko makubwa sana katika viwango vya ufaulu kwa mwaka 2018 ikilinganishwa na mwaka 2017 , ambapo mwaka huu 2018 , kwa ufaulu wa wastani wa GPA, kati ya shule 88 ni shule moja tu ambayo haijafikia watani wa 50, tofauti na mwaka 2017 ambapo shule zaidi ya 30 zilikuwa na  wastani  chini ya 50.


Naye Katibu tawala wa Mkoa wa Manyara ndugu Musa Musaile katika kikao chake na wakuu wa idara na vitengo wakati wa ziara yake wilayani hapa mwishoni mwa wiki ameipongeza sana wilaya ya Kiteto kwa ufaulu huo ambapo amesema kwamba Kiteto imejitahidi sana  kwa shule zake nyingi kuwa na ufaulu kwa zaidi ya 50%.Na kwamba shule iliyoshika nafasi ya kwanza kimkoa  ni kutoka wilaya ya Kiteto.


Mwagala pia amesema kwamba idara yake imejipanga kuhakikisha kwamba  kiwango cha ufaulu kinaendele kupanda mwaka hadi mwaka, na  ili kufanikisha hilo iko mikakati ambayo wameiweka ambayo itawawezesha kutimiza  lengo hilo.

Mwagala ameiainisha mikakati hiyo,  mkakati wa kwanza ukiwa ni kuwapa motisha walimu kwa kuwapongeza,kuwapa zawadi na kutambua kazi waliyoifanya ili waweze kujituma zaidi , mkakati wa pili ni kuanza maandalizi mwezi Januari mara tu shule zinapofunguliwa,kwa kuwapa wanafunzi wa darasa la saba mazoezi kwa wingi, mitihani kwa wingi, mkakati wa tatu ni kuwajengea walimu uwelewa zaidi katika mada wanazofundisha ili waweze kuwafundisha wanafunzi vizuri, na wanafunzi waweze kuelewa na mkakati wa nne ni kufanya ufuatiliaji wa karibu kila mara ili kuhakikisha kwamba walimu wanafundisha kulingana na maelekezo na malengo ambayo wilaya imejiwekea.



.....MWISHO.....

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • "VIJANA JIUNGENI KWENYE VIKUNDI ILI MUWEZE KUNUFAIKA NA MIKOPO YA 10%" - Ussi

    July 14, 2025
  • SEHEMU YA MICHANGO YA MWENGE YATUMIKA KUONGEZA NGUVU MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA.

    July 14, 2025
  • Bahati iliyoje! Mtoto Azaliwa Masaa Machache Kabla ya Uzinduzi wa Zahanati, Apewa Jina la Mkimbiza Mwenge.

    July 14, 2025
  • JESHI LA POLISI KITETO LAPONGEZWA KWA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

    July 14, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa