• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WAZEE WILAYANI KITETO WAOMBWA KUSAIDIA KUKEMEA UPOROMOKAJI WA MAADILI.

Imetumwa : October 1st, 2023


Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, SSI. Mbaraka Alhaji Batenga amewaomba wazee wilayani hapo kuisaidia serikali kukemea uporomokaji wa maadili katika jamii.

Ombi hilo limetolewa Oktoba 1,2023 katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani  yaliyofanyika katika Uwanja wa Michezo wa Wilaya uliopo Kibaya wilayani hapo.

Mh. Batenga amesema kwamba utandawazi unawamaliza vijana ila wazee wakishirikiana na serikali na jamii  kwa ujumla watafanikiwa kumaliza tatizo hilo.

“Kuna changamoto kubwa ya mporomoko wa maadili katika kizazi cha sasa  hivyo nitoe ombi kwa wazee mtusaidie kusimamia na kukemea uporomokaji wa maadili”, alisema Mh. Batenga.

Aidha Mh. Batenga alitumia jukwaa hilo kuwaasa vijana kutimiza wajibu wao katika kuwatunza wazazi wao kama ambavyo wazazi hao walivyowajibika kuwatunza vijana hao.

Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya, Mh Abdallah Bundala, aliwasihi wazee hao kuzingatia mazoezi ili kujiepusha na magonjwa yasiyo ambukiza kama vile kisukari na  shinikizo la damu.

Pia Mkurugenzi Mtendaji (W), CPA. Hawa Abdul Hassan, alisema kwamba ofisi yake ipo tayari muda wowote kwaajili ya kuwahudumia wazee hao  hivyo endapo watakua na changamoto yoyote na wakashindwa kuhudumiwa ipasavyo katika ofisi zilizo chini yake, wanakaribishwa katika ofisi yake na atawasikiliza.

Nae Mganga Mkuu wa Wilaya, Dr. Vicent Gyunda,  alisema  kwamba, kwa kutambua changamoto za afya zinazowakabili wazee, kwa sasa  hospitali ya wilaya imetenga madaktari wawili maalumu kwaajili ya kuwahudumia wazee tu ila katika vituo vya afya na zahanati hakuna madakatari waliotengwa kwaajili ya wazee hivyo huko utaratibu wa ‘mpishe mzee kwanza’  unatumika.

Katika maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya alikabidhi kadi za bima ya afya ya jamii iliyoboroeshwa kwa wazee kumi ambao watahitajika pia  kupeleka taarifa za wategemezi wao watano ili waweze kunufaika na huduma hiyo.

Maadhimisho hayo ambayo yalitanguliwa na matembezi ya hiyari, yalipambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo upimaji wa afya bure na michezo mbalimbali ambayo ilichezwa na wazee ikiwemo mchezo wa kukimbiza kuku, kuvuta kamba na maonesho ya mavazi na mchezo wa bao.

Katika zoezi la upimaji afya, wazee walipata fursa ya kupima macho na wale wote ambao walibainika na matatizo waliombwa kufika katika Hospitali ya Wilaya siku ya Terehe 10, Oktoba ,2023 kwaajili ya kupatiwa miwani. Aidha wazee hao walipata pia nafasi ya kupima shinikizo la damu, sukari, uzito na kupata ushauri mbalimbali wa afya kutoka kwa wataalamu wa afya wa wilayani hapo.

Akiongea kwa niaba ya wazee wengine, Mzee Habibu Hassan Surumbu alisema kwamba wamefurahi sana  kuona uongozi wa wilaya mwaka huu umewathamini na  kuwakumbuka kwenye siku yao hiyo muhimu kwa  kuandaliwa maadhimisho hayo maana walikua wanaona tu kwenye vyombo vya habari wilaya nyingine zikifanya maadhimisho hayo.

Katika kufunga maadhimisho hayo, Mkuu wa Wilaya aliwakumbusha wazee hao kuhusu mbizo za Mwenge wa Uhuru  wilayani hapo na kuwahimiza kujitokeza katika mbio hizo.

Wilaya ya Kiteto inatarajia kuupokea Mwenge wa Uhuru Oktoba 7,2023 katika eneo la Dosidosi ambapo Mwenge huo wa Uhuru utakuwa ukipokelewa Kimkoa kutoka katika wilaya ya Kongwa iliyopo mkoani Dodoma.

Matangazo

  • TAARIFA KWA UMMA 11.06.2025 June 11, 2025
  • TANGAZO NAFASI YA KAZI- MWENYEKITI BODI YA MFUKO WA ELIMU June 08, 2025
  • KUITWA KWENYE USAILI JUNI 2025 June 07, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 06, 2025
  • Angalia zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA MAANDALIZI YA MWENGE WA UHURU 2025

    June 11, 2025
  • WATOTO WA UMISSETA KITETO, WAWATOA JASHO WATU WAZIMA!

    June 10, 2025
  • WALIMU KITETO WAPEWA MAFUNZO YA AFUA JUMUISHI ZA ELIMU YA AFYA SHULENI

    June 05, 2025
  • AFYA NI MTAJI, TUJITOKEZE KWENDA KUPATA HUDUMA ZA KIBINGWA

    June 05, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa