Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh.Remedius Mwema Emmanuael ameagiza ifikapo Januari 15, 2024, wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na watoto wote waliofikia umri wa kuanza darasa la awali na darasa la kwanza, wawe wameshawasili shuleni kuanza masomo.
Mwema ameyaongea hayo Januari 8, 2023 wilayani Kiteto kwenye ziara ya kukagua na kuhakiki idadi ya wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza walioripoti shuleni.
Mh Mwema alisema kwamba serikali imebeba gharama za ada kwa wanafunzi wote hivyo hakuna sababu inayofanya mwanafunzi asiwepo darasani. “Na tulishatoa maelekezo kua hata kama mwanafunzi hana sare za shule au madaftari apokelewe wakati mzazi anaendelea kujipanga kukamilisha hayo mahitaji”’ aliongeza Mh. Mwema.
Aidha Mh Mwema alitoa maagizo kwa Maafisa Elimu Kata na watendaji wote wa vijiji na kata kuingia mitaani nyumba kwa nyumba kuhakikisha watoto wote waliofikia umri wa kuanza darasa la awali na la kwanza wamendikishwa na wanaenda shule na wale waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wote nao wameripoti shuleni.
“Upande wa wale waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza, nahitaji orodha ya wote ambao hawajaripoti shuleni na kila mtoto nipewe sababu kwanini hayupo darasani nahitaji na namba ya simu ya mzazi au mlezi”, alisema Mwema.
Vilevile, Mh Mwema alimuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto, kuanza kukamata wazazi/walezi ambao watoto wao watakua hawajaripoti shuleni kuanzia Januari 15, 2024.
Mbali na kuweka juhudi kwa wanafunzi hao wapya, Mh Mwema pia aliagiza kwamba wanafunzi wanaoendelea nao wafuatiliwe kama wote wamerudi shuleni ili kuthibiti wanafunzi kuacha shule.
Katika ziara hiyo ambayo Mkuu wa Wilaya aliambatana na wataalamu mbalimbali wa halmashauri pamoja na Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi Kiteto, alikagua shule nne za msingi ambazo ni Boma, Kibaya, Chemchem na Kijungu. Upande wa shule za sekondari ni Kiteto na Kibaya.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa