• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Walimu Waaswa Kutoiweka Rehani Michezo

Imetumwa : November 7th, 2018

Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwatunuku vyeti pamoja na kufunga mafunzo ya michezo ya riadha kwa watoto ' Kids athletics' Ndg. Fidelis Kyarwenda akizungumza na walimu walioshiriki mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwenye uwanja mkuu wa michezo  uliopo  katika  mji mdogo wa Kibaya, wilayani  Kiteto, Mkoa wa Manyara.

Afisa michezo ( W) bibi Juliana Mtei akizungumza wakati wa hafla hiyo.



..........HABARI KAMILI...........



Mgeni rasmi katika hafla fupi ya kuwatunuku vyeti pamoja na kufunga mafunzo ya michezo ya riadha kwa watoto ' Kids athletics' ambaye pia ni Mdhibiti mkuu wa ubora wa shule wilaya ya Kiteto ndugu Fidelis Kyarwenda  amewataka walimu kutouweka mifukoni ujuzi walioupata kupitia mafunzo hayo,badala yake waende wakawafundishe wanafunzi wao.Kyarwenda ameyasema hayo  Jumatatu  ya  tarehe 05/11/2018 katika uwanja mkuu wa michezo  uliopo  ndani ya mji mdogo wa Kibaya, wilaya ya Kiteto, Mkoani wa Manyara.


Akizungumza wakati wa hotuba yake Kyarwenda amesema “ mmeahidi wenyewe hapa kwamba mafunzo mliyoyapata hamtayaweka mifukoni,bali mtakwenda kuwafundisha wanafunzi wenu.Mkifanya hivyo hamtakuwa mmeiweka rehani michezo, watoto wetu watacheza. Msiende kutafuta sababu ya kuhalalisha kutowafundisha watoto, mkafundishe watoto na kuwasimamia kama mlivyofundishwa na kusimamiwa  hadi mkaelewa”.


Kyarwenda  ameendelea kusema kwamba michezo ambayo walimu hao wamejifunza, wakienda kuifundisha katika shule zao, na watoto wakaelewa ,wataipenda , ari ya kupenda shule itaongezeka, itakuwa chachu ya kupunguza utoro shuleni, kwa sababu hata  watoto wasiopenda kwenda shule, wasiofanya vizuri darasani ,michezo itawavuta kwenda shule .


Kyarwenda amesema kwamba kazi yake ni kusimamia ubora wa elimu, na kwa sababu michezo mashuleni ni sehemu ya elimu, atasimamia kikamilifu kuhakikisha kwamba michezo hiyo inafundishwa katika shule zote ambazo zimeleta walimu kwenye mafunzo hayo. Aidha   amemuomba Afisa michezo wa wilaya kumpatia orodha ya washiriki wote wa mafunzo, ili atakapokuwa anakwenda kufanya ukaguzi ,afuatilie kama wanafunzi wanafundishwa michezo hiyo.


Kadhalika Kyarwenda amewataka walimu hao  kujenga mahusiano mazuri mahali popote pale watakapokuwa.Amesema kwamba wamejifunza michezo uwanjani, lakini pia wamejifunza mambo mengi, wameona jinsi mkufunzi wao alivyo na mahusiano mazuri na watu, hadi kufikia hatua ya kuwatafutia nafasi za chuo kwa wale watakaokuwa tayari kujiendeleza katika fani ya michezo,na wao wanapaswa kuwa na mahusiano mazuri, ili pale wanapokuwa wanahitaji kufanya jambo fulani waweze kulifanya kwa urahisi.


Kyarwenda pia amewasifu walimu hao kwa nidhamu waliyoionyesha wakati wote wa mafunzo. Amewaambia kwamba walitumwa kujifunza michezo ili wakafundishe wanafunzi, wamefanya mafunzo vizuri, wamekuwa na nidhamu wakaweza kujifunza, hivyo kwa uwiano huohuo, nidhamu hiyohiyo ambayo wameionyesha wakati wa mafunzo, wakaionyeshe katika kuwafundisha wanafunzi wao ili matunda ya mafunzo hayo yaonekane kwenye shule zao.


Kyarwenda pia amezungumzia suala la vifaa vya michezo, amesema kwamba vifaa vyote ambavyo vimetumika katika mafunzo hayo ni vya kisasa, vifaa ambavyo katika mazingira wanakotoka walimu hao havipo, lakini wao kama walimu wanatakiwa kufaragua zana za kufundishia, wakafarague vifaa vya kufundishia  michezo hiyo, watoto wasiache kucheza kwa sababu vifaa hivyo havipo.


Sambamba na kuwataka walimu hao kufaragua vifaa vya kufundishia michezo hiyo, Kyarwenda amesema kwamba suala la kuwa na vifaa  vya michezo ni la muhimu, hivyo atashirikiana na Afisa michezo wa wilaya kulipeleka suala hilo kwa Mkurugenzi ili kwa pamoja waone ni kwa namna gani vifaa hivyo vinaweza kupatikana .


Naye afisa michezo wa wilaya ya Kiteto mama Juliana Mtei,ameahidi kuyasimamia na kufuatilia yote ambayo wamekubaliana katika mafunzo hayo.Huku akisisitiza kwamba walimu wote ambao wameshiriki katika mafunzo hayo,watapewa kipaumbele wakati wote ambapo  mafunzo na shughuli mbalimbali za michezo zitakuwa zikifanyika,iwe ndani ya wilaya au za kwenda nje ya wilaya.

Katika hatua nyingine walimu walioshiriki mafunzo hayo wameshukuru kwa kupata fursa ya kushiriki, pia wamemshukuru mkufunzi kwa kazi nzuri aliyoifanya, kazi ambayo imewawezesha kufahamu michezo mingi,ambayo kabla ya mafunzo hayo hawakuwa wakiifahamu.Aidha wamemuomba asiache kufika Kiteto kutoa mafunzo ,kila wakati anapopata nafasi,kwani wanaamini kwamba bado anayo mengi ya kuwafundisha, ili waweze kuwa walimu bora wa michezo kwa siku za usoni.


Kwa mara ya kwanza walimu  kutoka shule za msingi na sekondari wilayani  hapa wameweza kukusanyika pamoja na kupata mafunzo mbalimbali ya michezo ya watoto.Jumla ya walimu 91 wameshiriki mafunzo hayo ya siku tatu  na kutunukiwa vyeti .



.......MWISHO..........


Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa