• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Walimu 91 Kiteto Wapatiwa Mafunzo ya Michezo ya Riadha kwa Watoto ‘Kids Athletics’

Imetumwa : November 6th, 2018

Afisa michezo wa mkoa wa Manyara ambaye pia ni mkufunzi wa mafunzo  ya riadha kwa watoto 'Kids Athletics', Ndg. Charles Maguzu akizungumza  wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika uwanja Mkuu wa michezo Kibaya - Kiteto .

Walimu kutoka katika shuke mbalimbali wilayani Kiteto wakiwa tayari kuanza na mafunzo ya michezo ya riadha kwa  watoto ' Kids Athletics'.

Walimu Rodgers  Mvigilije wa shule ya sekondari Kiteto na Edna Tesha wa shule ya msingi Songambele wakitoa maoni yao kuhusiana na mafunzo waliyoyapata.



.......HABARI KAMILI.........



Walimu 91 wa shule za msingi na sekondari wilayani hapa wamepata mafunzo ya michezo mbalimbali .Mafunzo hayo ya siku 3 yamefanyika kwenye uwanja mkuu wa michezo katika mji mdogo wa Kibaya,wilayani Kiteto, ambapo yalifunguliwa rasmi siku ya Jumamosi 03/11/2018 na kufungwa  jana Jumatatu  05/11/2018.


Akizungumza kuhusu mafunzo hayo,Afisa michezo wa mkoa wa Manyara ambaye pia ndiye mkufunzi wa mafunzo hayo, ndugu Charles Maguzu amesema “ Mafunzo haya niliyapata Dar es Salaam, chini ya  Shirikisho la Michezo ya riadha la Dunia (IWF).Lengo la mafunzo haya ni  kuwafundisha walimu michezo michezo  ili waweze kwenda kufundisha  michezo hiyo katika shule zao.Riadha ndio mchezo mama wa michezo yote,katika michezo yote ambayo tunacheza, watu lazima wakimbie,lazima waruke,lazima warushe.Ndani ya mchezo wa riadha matukio yote hayo yamo. Kwa hiyo tunawapa 'kids athletics program' ambazo zitatengeneza msingi wa kuwafanya waweze kufundisha michezo yote ,kwa ajili ya kukuza vipaji vya watoto”.


Aidha Maguzu  ameeleza umuhimu wa michezo ambapo amesema kwamba michezo inaongeza nidhamu kwa wanafunzi mashuleni . Inawajenga kiafya. Inawajengea uwezo wa kujiamini na kuwa wadadisi wa mambo.Wanakuwa na uwezo wa kupambana katika mazingira yoyote yale.Michezo pia inajenga ushirikiano miongoni mwa wanafunzi wanapokuwa wanasoma. Na kwamba wanaposoma kwa ushirikiano,uelewa wao unakuwa mpana zaidi.Pia inajenga upendo kwa wanafunzi, kukutana  pamoja na kucheza  kunawafanya wajione kama ndugu.


Maguzu ameongeza kusema kwamba kila mwalimu aliyeshiriki katika mafunzo hayo, anatakiwa akafundishe wanafunzi wasiopungua 350,na kwa kufanya hivyo ,wanafunzi wengi katika  wilaya ya Kiteto wataweza kupatiwa mafunzo hayo.anaamini kuwa  walimu ambao wamepata mafunzo hayo wakiyapeleka kwa wanafunzi , kuanzia mwakani wilaya ya Kiteto itakuwa inatengeneza wanafunzi ambao wanavipaji  na ujuzi wa kutosha kufanya vizuri katika UMITASHUMTA na UMISETA na kuiletea sifa wilaya yao.


Katika hatua nyingine Maguzu ametoa shukrani kwa Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi Mtendaji  kwa kuhamashisha  walimu kujitokeza kwa wingi kushiriki mafunzo hayo.Vilevile amewasifu walimu kwa kushiriki mafunzo vizuri, pamoja na kuonyesha nidhamu  ya hali ya juu katika siku zote  za mafunzo .


Sambamba na shukrani hizo amewaasa walimu  kwamba baada ya kupata mafunzo hayo na kutunukiwa vyeti, wasiende kuvifungia kabatini na kutowafundisha  watoto ,endapo watafanya hivyo ,watakuwa hawajayatendea haki mafunzo hayo, wala wanafunzi wao, na lengo la kushiriki mafunzo litakuwa halijatimia. Vilevile Maguzu ametoa wito  kwa walimu waliohudhuria mafunzo hayo ambapo amesema kwamba wajipange wakati mwingine pia waweze kuhudhuria mafunzo.Na kwa kuwa wilaya ya Kiteto ni kubwa, hata kama wataamua kujipanga huko pembezoni mwa mji,atakuwa  tayari kuja kuwafundisha, kwani lengo lake lengo ni kuwafikia walimu wengi , ili mafunzo hayo yawafikie  watoto wengi zaidi.


Kwa upande wao walimu waliopata mafunzo hayo walikuwa na haya ya kusema;

Mwalimu Edna Tesha wa shule ya msingi Songambele amesema kwamba amefurahia sana mafunzo aliyoyapata ,kwani yamemsaidia kuimarisha afya yake, amejua uwezo wake katika michezo ,pia yamemsaidia kufahamu michezo mingi ambayo atakwenda kuwafundisha wanafunzi wake. Mwalimu Tesha anaamini kwamba michezo hiyo itawasaidia watoto kuwa imara, kuwa na akili ya kujifunza  na kuelewa kwa haraka. Pia  ameiomba Halmashauri chini ya Mkurugenzi ; mafunzo yatolewe mara kwa mara ili walimu wawe na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kuandaa kizazi chenye vipaji na ujuzi wa kucheza michezo mbalimbali.


Mwalimu Rogers Mvigilije  wa shule ya sekondari Kiteto amesema kwamba  mafunzo yalikuwa mazuri sana, wamejifunza vitu vingi , wamejifunza michezo mbalimbali, kila aina ya mchezo ambao watoto wanastahili kufundishwa wameugusa. Mwalimu Mvigilije pia amesema kwamba anaamini kuwa mafunzo waliyopata yataisaidia jamii. Vilevile ametoa rai kwamba mafunzo yawe endelevu, na kwamba Halmashauri iendeelee kuona ni kwa namna gani wakufunzi wa michezo wataendelea kuja Kiteto ili walimu waendeelee kupata ujuzi zaidi na zaidi kwa lengo la kuinua michezo wilayani.



..........MWISHO.........

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa