• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wakuu wa idara Watakiwa Kushirikiana katika Uandaaji wa Bajeti ya Masuala ya Lishe

Imetumwa : November 29th, 2018

Mwezeshaji wa mafunzo ya awali ya mipango na bajeti ya masuala ya lishe ngazi ya halmashauri  bibi Stella Sasita akielekeza kuhusiana na mambo  ya msingi ya kusisitiza wakati wa uandaaji wa bajeti katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hospitali ya wilaya ya Kiteto mwishoni mwa wiki.

 Mwezeshaji wa mafunzo  Ndg. William Mambo akielekeza kuhusana na mfumo wa Plan Rep na mabadiliko yaliyofanyika.

Afisa lishe ( W) ya Kiteto Bibi Beatrice Rutanjuka akiwasilisha taarifa yake ya shughuli za lishe kabla ya kuanza kwa mafunzo.

Washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja,mara baada ya kumaliza mafunzo.



.......HABARI KAMILI .......






Wakuu wa idara zinazohusika na masuala ya lishe  katika Halmashauri ya wilaya ya Kiteto wametakiwa kushirikiana katika uandaaji wa bajeti ya shughuli za lishe.Kauli hiyo imetolewa na muwezeshaji wa mafunzo ya awali ya mipango ya bajeti ya masuala ya lishe ngazi ya halmashauri  bibi Stella Sasita  wakati wa kikao kazi cha mafunzo hayo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hospitali ya wilaya  mwishoni mwa wiki.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa ushirikiano katika uandaaji wa bajeti na  mipango kazi  ya shughuli za lishe Sasita amesema “ Mipango iwe ya ushirikiwaji.Wakuu wa idara mshirikiane, ushirikishwaji unaondoa kujirudia rudia kwa shughuli katika mipango kazi. Kwamba kama mwenzako amepanga kutekeleza shughuli fulani,kwa sababu amekushirikisha, wewe hutaiweka tena kwenye mpango wako,utaweka shughuli nyingine’’.

Sasita pia amefundisha kuhusu mambo muhimu yanayotakiwa kutiliwa mkazo wakati wa uandaaji wa bajeti na mipango ya shughuli za lishe, Sasita  amesema kwamba ili kupanga ni lazima kuwa na takwimu.Takwimu ni muhimu sana . Kuwa na malengo ambayo ni  ‘SMART’ kwa maana kwamba malengo  yanatakiwa kuwa  maalum,yanayopimika,yanayotekelezeka,yawe na uhalisia na muda maalumu wa utekelezaji.

Aidha Sasita ameelekeza kwamba shughuli zote zinazohusiana na masuala ya lishe zinatakiwa zilenge kwenye lengo J. Si hivyo tu, bali  shughuli zote za masuala ya lishe ambazo zitapangwa , ni lazima pia zilenge  kusaidia utekelezaji wa mkataba uliosainiwa na Katibu Tawala wa Mkoa.  Sasita amesema kwamba mambo ya kufanya ni mengi sana ,na kwamba kikao hicho ni cha utekelezaji,kinahitaji matokeo hivyo wakuu hao wa idara waongeze bidii zaidi  ili kuweza kupata matokeo chanya katika utekelezaji wa shughuli za lishe.

Naye mwezeshaji William Mambo ameeleza kuhusu mabadiliko  yaliyofanywa katika mfumo wa Plan Rep ambapo amesema kwamba mwaka wa fedha uliopita shughuli nyingi za lishe zilikuwa katika lengo C, lakini baada ya mabadiliko shughuli hizo kwa sasa  zipo katika lengo J. Na kwamba afisa mipango ana jukumu la kuhakikisha kwamba taarifa zote zinaingia kwenye mfumo.Amesisitiza kuwa ni lazima  wakuu wa idara  pamoja na maafisa bajeti wote kujua kwamba shughuli zao zinatekelezwa kwenye nini. Mambo pia amekazia kuhusu suala la ushirikano,ambapo amesema kwamba wakuu wa idara na maafisa bajeti washirikiane wakati wa kuandaa bajeti, ili kuwa na uhakika kwamba shughuli walizokusudia kuzitekeleza zimeingizwa kwenye mfumo.

Katika hatua nyingine Afisa lishe wa wilaya ya Kiteto bibi Beatrice Rutanjuka amesisitiza kuhusu mabadiliko katika ufuatiliaji wa bajeti,ambapo amewataka wakuu wa idara kuhakikisha kwamba  hawaishii tu kwenye kupanga bajeti ya shughuli za lishe katika idara zao, bali pia wawe wafuatiliaji kuhakikisha kwamba fedha  zilizotengwa zinapatikana, na utekelezaji wa shughuli unafanyika kama inavyoonekana katika mipango yao.

Vilevile  Rutanjuka amezungumzia kuhusu suala la kujituma ,amesema kwamba ni muhimu sana  kila mmoja kujituma ili mambo yaweze kwenda,kwani bila ya kuwa na moyo wa kujituma hakuna jambo lolote litakalofanikiwa .

Mafunzo hayo ya siku moja yamelenga katika kuzijengea uwezo kamati za lishe , kupanga na kusimamia masuala ya lishe  ngazi ya wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa Tanzania Bara.






.........MWISHO..........



Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa