• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WADAU WAJIPANGA KUHAKIKISHA MFUMO WA STAKABADHI GHALANI MSIMU HUU UNAFANIKIWA ZAIDI.

Imetumwa : May 23rd, 2024

Timu ya wataalamu kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Mei 22,2024 imetembelea Wilaya ya Kiteto na kufanya kikao kujadili changamoto zilizojitokeza katika uuzaji wa zao la mbaazi kupitia Mfumo wa Stakabadhi  Ghalani katika msimu uliopita.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mh. Remidius Mwema, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto CPA. Hawa Abdul Hassan, wajumbe wa Kamati ya Fedha, wataalamu wa kilimo kutoka ofisi ya Mkoa na kutoka  Wilayani Kiteto, pamoja na maafisa ushirika wa Wilayani hapo.

                                                                                                          

Katika kikao hicho, wadau hao walijadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza katika uuzaji wa zao la mbaazi katika msimu ulipita na kujadili njia za kutatua changamoto hizo ili kuziepuka katika msimu huu.

Kati ya changamoto zilizojitokeza katika msimu uliopita ni pamoja na upungufu wa maghala ya kutosha katika vyama vya msingi vya  mazao na masoko yenye kukidhi vigezo vya kuhifadhia mazao, uelewa mdogo wa wakulima kuhusu  mfumo wa stakabadhi ghalani na uwepo wa walanguzi/madalali ambao walikua wananunua mbaazi moja kwa moja kutoka kwa wakulima.

                                                                                                                                             

Aidha changamoto nyingine ni kutokuwepo na mageti  ya kutosha  kwenye mipaka ya wilaya ya Kiteto ili kuzuia utoroshwaji  wa mbaazi kutoka nje ya wilaya na pia baadhi ya vyama vya msingi kutokua tayari kuingia kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani.

Katika kutatua changamoto ya utayari wa vyama vya msingi, wajumbe walikubaliana maafisa ushirika wakae na vyama vya msingi wajue kuhusu utayari wao kuingia kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani na pale itakapoonekana hawapo tayari, ijulikane nani atafanya kazi kwa niaba yao.

Aidha wajumbe wamekubaliana kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mfumo huo kwani katika msimu uliopita zoezi lilianza mwishoni wa msimu na hivyo hakukua na muda wa kutosha wa kutoa elimu hiyo kwa wakulima.

Vilevile imejadiliwa kuwekwa mageti ya kutosha haswa maeneo ambayo yanapakana na wilaya nyingine ili kudhibiti utoroshwaji wa mbaazi.

Kuhusu changamoto ya maghala, Bi Sura Ngatuni, Meneja wa Mipango na Uhamasishaji WRRB, amesema kwamba WRRB itatuma wataalamu kukagua maghala ya watu binafsi ili kubaini kama yanakidhi vigezo ili yaweze kuongezwa kwaajili ya kurahisha ukusanyaji wa mbaazi.

                                                                                                           

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa