Kikao cha ndani cha kamati ya Lishe ya Wilaya kilichofanyika tarehe 21/10/2022 kilikuwa mahususi kwa ajili ya uwasilishwaji wa taarifa za utekelezaji wa shughuli za lishe kwa kipindi cha robo ya Kwanza(Julai- Septemba 2022).
Katika kikao hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bwana Christopher Simwimba ajenda zipatazo saba (7) zilijadiliwa na taarifa zipatazo 13 kutoka kwa wajumbe mbalimbali wa kikao hicho ziliwasilishwa kwa ajili ya kuonesha utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe zilizofanyika ndani ya Halmashauri.
Katika taarifa hizo mafanikio mbalimbali yalianishwa kwa kila idara iliyowasilisha taarifa yake lakini pia changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wa shughuli za lishe na hatua za kuzitatua zilizochukuliwa.
Aidha wakati akifunga kikao hicho Mwenyekiti wa kikao Bwana Christopher Simwimba aliwasihi wajumbe kusimamia maadhimio wanayojiweke pamoja na kusimamia sheria wakati wa utekelezaji wa shughuli za lishe na kuongeza ufuatiliji ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea.
Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Lutanjuka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe kwa Kitengo cha Lishe.
Wajumbe wa kikao cha kamati ya lishe Wilaya
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa