Wakazi wa Kata ya Kijungu Wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti Kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Kata Hiyo Wilayani Kiteto
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti Akizungumza na Baadhi ya Wananchi Mara Baada ya Mkutano wa Hadhara Uliofanyika Katika Kata ya Kijungu Wilayani Kiteto
RC Mnyeti Avunja Uongozi wa Kijiji
Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti ameuvunja uongozi wa kijiji cha Kijungu kilichopo katika kata ya Kijungu wilayani Kiteto baada ya kugundua kuwa kuna matumizi yasiyoeleweka ya fedha za kijij yaliyofanywa na uongozi huo wakishirikiana na diwani wa kata ya Kijungu bibi Mandalo Mussa. Tukio hilo limetokea katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Kijungu wilayani Kiteto.
Akiwa katika mkutano huo Mhe. Mnyeti alimtaka mwenyekiti wa kijiji hicho kutoa maelezo kuhusu fedha hizo za kijiji , ambapo maelezo yake yalisababisha Mhe. Mnyeti kutoa amri ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo kwa tuhuma za kushiriki katika wizi wa fedha za wananchi. Kadhalika Mhe. Mnyeti aliwaita wajumbe wote wa serikali ya kijiji, na kuwahoji kuhusu fedha hizo .Hata hivyo maelezo yao yalimsababisha Mhe. Mnyeti kufikia maamuzi ya kuuvunja uongozi wa kijiji hicho. Akizungumza wakati anatoa maamuzi hayo Mhe. Mnyeti anasema ‘‘Nimeuvunja rasmi uongozi wa kijiji hiki.Hatuwezi kuwa na viongozi ambao wanaiba fedha za wananchi. Mkurugenzi itisha uchaguzi mara moja kijiji hiki kipate uongozi mwingine”.
Katika kata ya Kijungu kumekuwa na mgogoro ambao umedumu kwa muda sasa kati ya Mhe. diwani wa kata hiyo na mwenyekiti wa kijiji cha Kijungu ,mgogoro unaohusisha matumizi ya fedha za kijiji ambayo yanadaiwa kufanywa na Mhe. Diwani wa kata ya Kijungu kinyume na makubaliano yaliyokuwepo kati ya uongozi wa kijiji hicho na Mhe. diwani, hali ambayo imesababisha Mhe. diwani huyo kukamatwa na kuwekwa mahabusu siku chache kabla ya ziara ya Mhe. Mnyeti katika kata hiyo.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa