• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Naibu Waziri Waitara Awataka Watumishi Kuwajibika

Imetumwa : December 15th, 2018

Naibu Waziri wa OR- TAMISEMI Mhe. Mwita M. Waitara akizunguza  katika kikao chake na watumishi  kilichofanyika ndani ya ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto mapema leo.Waliokaa upande wa kulia ni mwenyekiti wa halmashauri Mhe. Lairumbe Mollel na upande wa kushoto ni kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Christopher Simwimba.

Katibu Tawala Ndg. Musa Waziri akimkaribisha Naibu waziri kuzungumza  na watumishi.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto  Ndg. Christopher Simwimba akitoa akitambulisha watumishi.



............HABARI KAMILI..................



Naibu waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ( TAMISEMI) Mheshimiwa Mwita Waitara amewataka watumishi kuwajibika katika nafasi zao.Mheshimiwa Waitara ameyasema hayo wakati wa kikao chake na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto  kilichofanyika mapema  leo tarehe 15.12.2018 katika ukumbi wa Halmashauri .


Akizungumza katika kikao hicho Mheshimiwa Waitara amewaasa watumishi kuhusu kufanya kazi kwa bidii ,sambamba na kufuata taratibu ,hapa Mhe. Waitara anasema “ Wito wangu kwenu watumishi, kila mtu awajibike kwenye nafasi yake.Serikali inataka watumishi wafanye kazi .Msifanye siasa kazini.Acheni maneno maneno.Usicheze ngoma ambayo sio ya kwako,suala la utumishi ni suala binafsi.Mtu hata kama amelipwa jana,akigundua kama unataka kumkopa atakwambia sina hela.Kila mtu ana namba yake ya ajira.Kama una madai au malalamiko, kuna taratibu za kufuata. Sio sawasawa kufanya kazi chini ya kiwango kwa sababu una madai”.


Mheshimiwa Waitara amesema kwamba kupandishwa vyeo, kuna vigezo. Na kwamba wao kama serikali wanafahamu kwamba idara nyingi zina malamiko , hususani idara ya elimu , walimu wanalalamika kwamba hawapandishwi madaraja, lakini pia wanafahamu kwamba kuna watumishi hawatimizi wajibu wao, hawafanyi kazi. Lakini pia wanafahamu kwamba wako watumishi wazuri sana Halmashauri lakini hawapandishwi madaraja kwa sababu kuna watu wanawafanyia wenzao roho mbaya, taarifa hazikamiliki,kwa hiyo mtumishi anakaa anasubiri kupandishwa cheo, lakini hapandishwi cheo.


Kadhalika Mhe. Waitara amesema kwamba wameelekeza wakuu wa idara kuwa wajipangie ratiba,kupunguza umbali , wafike ofisi za kata wakawasikilize watumishi walioko huko ,wasisubiri watumishi hao wawafuate. Kadhalika amewataka wakuu hao wa idara  kuwa wabunifu katika kushughulikia masuala mbalimbali katika idara zao,wawe watatua matatizo, wasiwe wa kulalamika kama watumishi walio chini yao, watatue matatizo, yale yatakayokuwa yanawashinda ndio wayapelekwe kwa Mkurugenzi  na kutokea kwa Mkurugenzi yatafika katika ngazi nyingine za juu kwa utatuzi.

 Mheshimiwa Waitara pia amezungumzia kuhusu lugha ambazo zinatumika kwa watumishi ,ambapo amesema kwamba kuna Halmashauri nyingine maafisa utumishi wana lugha ambazo sio nzuri kwa watumishi.Amesema kwamba  kama wanaona  watumishi wanazungumza au kufanya mambo ambayo sio sahihi , kazi yao ni kuwaelewesha kwa sababu wao wanaelewa zaidi kuliko watumishi wengine.


Aidha Mheshimiwa Waitara ametoa maelekezo kuhusu watumishi wa idara ya afya kulipwa shilingi 120,000/= kila mwaka kwa ajili ya sare za kazi.Amesisitiza kwamba maelekezo hayo yametokana na agizo la Waziri Mkuu Mhe Kasim Majaliwa ambaye ameagiza kuwa kabla ya mwaka 2018 kwisha watumishi hao wawe wamelipwa fedha hizo ambazo ni kutoka katika mapato ya ndani ya Halmashauri.


Katika hatua nyingine Mheshimiwa Waitara ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Kiteto kwa  ukusanyaji mzuri wa mapato ,ambapo amesema kwamba katika mkoa wa Manyara ,wilaya ya Kiteto ndiyo inaongoza . Vile vile ameipongeza kwa kiwango kizuri cha ufaulu ambapo amesema kwamba pamoja na kuwa wilaya ni ya wafugaji, lakini inafanya vizuri kwenye elimu,jambo ambalo ni la kupongezwa sana.


Katika kikao hicho Mhe Waitara amezungumzia kuhusu mambo mbalimbali ikiwemo maadili ya utumishi wa umma, ushirikiano kati ya watumishi na wakuu wa idara, utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya serikali,utii wa sheria na kanuni za nchi, pamoja na wajibu wa viongozi katika utatuzi wa migogoro baina ya wakulima na wafugaji.




............MWISHO..............




Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa