Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) Wapata Mafanikio Makubwa Wilayani Kiteto.
Imetumwa : June 27th, 2017
Mh.Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Ndg. Tumaini Magesa ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN) wakati wa zoezi la utoaji za Vitambulisho vya Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa (iCHF) Zoezi hilo lilifanyika katika Ofisi ya Kijiji cha chapakazi kata ya chapakazi. Waliombatana na Mkuu wa Wilaya kushoto kwake ni Mh.Lailumbe Mollel Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kiteto na Diwani wa Kata hiyo ya Chapakazi,kulia kwake ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Jamii na Diwani wa Dosidosi Mh. Hassan Benzi.
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (PSSN) Wapata Mafanikio Makubwa Wilayani Kiteto
Mpango wa kunusuru kaya maskini (PSSN) umepata mafanikio makubwa wilayani Kiteto ambapo kaya 4835 zimejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii . Walengwa wa PSSN kujiunga na mfuko wa iCHF ni mafanikio makubwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) kwani kupata uhakika wa huduma za afya na matibabu ni nyenzo muhimu katika kuziwezesha kaya masikini kujikwamua kiuchumi. Mafanikio mengine ni pamoja na mahudhurio kwenye shule na vituo vya afya (kliniki) kuongezeka hususani kwa watoto wanaotoka kwenye kaya zinazonufaika na mpango.Pia walengwa wameboresha makazi yao kwa kujenga nyumba bora na wengine kukarabati nyumba zao . Kaya 4320 zimeanzisha miradi ya kiuchumi kama vile ufugaji kuku, bata, nguruwe na mbuzi na kujiunga kwenye vikundi vya kuweka na kukopa kutokana na pesa zinazotolewa na mfuko ambapo Kiasi cha shilingi 70,976,970.00. Kati ya kiasi hicho shilingi 69,787,000.00 (88%) zimelipwa kwa walengwa na shilingi 1,189,970.00 (1.5%) zimetolewa kwenye vijiji kwa ajili ya uwezeshaji na usimamizi kaya 159 zinanufaika ambapo vijiji vya Chapakazi na Asamatwa ni miongoni mwa vijiji 39 vinavyonufaika na mpango huu.
Pamoja na mafanikio yaliyopatikana, PSSN inakabiliwa na changamoto kadhaa kama vile baadhi ya walengwa kutumia isivyostahili ruzuku inayotolewa mfano kunywea pombe, kuongeza wake na baadhi ya wanaume kuwanyang`anya fedha wake zao ambao ndio wawakilishi wa kaya na kuzitumia katika matumizi yasiyo na tija.
Aidha Katika kukabiliana na changamoto hizo hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwemo halmashauri kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji kubadilisha wawakilishi wa kaya.Pia Ofisi ya TASAF kwa kushirikiana na uongozi wa vijiji na kamati ya usimamizi kutoa elimu kwa walengwa ili kutumia ruzuku kwa njia ya tija na endelevu.