Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti akitoa maelekezo kuhusu SULEDO katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanya vya soko, kata ya Sunya - wilayani Kiteto
Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa akitoa ufafanuzi kuhusu mwongozo wa SULEDO katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanya vya soko, kata ya Sunya - wilayani Kiteto
Wakazi wa kata ya Sunya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Alexander Mnyeti alipokuwa akizungumza nao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanya vya soko, kata ya Sunya.
...................HABARI KAMILI..............
Mkuu wa Mkoa wa Manyara atoa Siku 14 Kupatikana Uongozi Mpya wa Hifadhi ya Msitu wa SULEDO Kiteto
Mkuu wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Alexander Mnyeti amemuagiza mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magessa kusimamia na kuhakikisha kwamba hifadhi ya Msitu wa SULEDO inapata uongozi mpya ndani ya siku 14.Mhe. Mnyeti ametoa agizo hilo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya soko, kata ya Sunya wilayani Kiteto.
Agizo hilo la Mhe. Mnyeti limekuja baada ya wananchi wengi kulalamika juu ya ubadhilifu unaofanywa na viongozi wa hifadhi hiyo ,ambapo baadhi yao wamesema kwamba hawaelewi maana ya msitu huo wa SULEDO kwa sababu haunufaishi vijiji vinavyounda hifadhi hiyo,badala yake unanufaisha watu wachache ambao ni viongozi wa hifadhi hiyo. Kwani mauzo yanayotokana na mazao ya Hifadhi hiyo hayajulikani yanakokwenda wala yanavyotumika. Vilevile wananchi wa Sunya wamesema kwamba hawaelewi mipaka halisi ya Msitu wa SULEDO kwani wamekuwa wakiamriwa kuondoka kwenye mashamba yao wakiambiwa kwamba ni maeneo ya hifadhi hali ya kuwa wao ni wamiliki wa mashamba hayo kabla ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo. Kufuatia malalamiko ya wakazi wengi wa kata ya Sunya, Mheshimiwa Mnyeti anatoa agizo anasema ‘‘ malalamiko ya wananchi yanapokuwa mengi sana yanajenga chuki kati ya wananchi na serikali yao.Sasa mimi natoa agizo, mkuu wa wilaya nakupa siku 14 kushughulikia suala la SULEDO.Kuanzia sasa uongozi wa SULEDO nimeuvunja .Halafu sasa kasimamie uongozi mpya upatikane ndani ya hizo siku 14”.
Aidha Mhe. Mnyeti ameelekeza utaratibu utakaotumika katika kuchagua uongozi wa hifadhi hiyo ambapo amemtaka Mkuu wa wilaya ya Kiteto mheshimiwa Tumaini Magessa kusimamia mchakato wote wa upatikanaji wa uongozi huo mpya. Hapa Mhe. Mnyeti anasema‘‘.Nenda kasimamie upatikanaji wa wajumbe watatu watatu kwenye kila kijiji.Nataka wewe ndio uende kwenye hiyo mikutano kwenye kila kijiji, uhakikishe akidi imetimia ,mwenyekiti yupo ,mtendaji wa kijiji yupo, wananchi wachague wenyewe kwamba sisi tunamwamini fulani na fulani watuwakilishe kwenye SULEDO katika vijiji vyote 13”.
Katika hatua nyingine Mhe. Mnyeti pia amemtaka Mhe. Magessa kuhakikisha kwamba baada ya kupatikana kwa uongozi mpya wa msitu huo , Afisa misitu na afisa wa Wakala wa Huduma za Misitu ( TFS) wanatoa semina kwa uongozi huo kuwafundisha namna wanavyoweza kusimamia msitu wao,ili msitu huo uwanufaishe wananchi wote,kwani usipowanufaisha wote. Wananchi watauharibu. Akisisitiza juu ya umuhimu wa hifadhi hiyo kuwa na manufaa kwa wananchi wote, Mhe. Mnyeti anasema ‘‘Msitu huu usipowanufaisha wananchi wote,wataanza kuuharibu , na wakiuharibu serikali itawakamata, na ikiwakamata wananchi wanajenga chuki na serikali yao hali ya kuwa wataalamu wapo na watawala tupo”.
Msitu wa SULEDO ni msitu ambao umeundwa na kata tatu za Sunya ,Lengatei na Dongo ambapo wananchi toka vijiji 13 vya kata hizo walitoa ardhi ya vijiji vyao na kutenga kuwa msitu wa hifadhi ya jamii.
............... MWISHO...............
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa