Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kiteto (aliyeshika mfagio kushoto) Ndg. Tamim H. Kambona akijumuika na watumishi wengine katika kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Wilaya - Kiteto, Mjini Kibaya leo siku ya Uhuru 09.12.2018. Kulia kwake ni Mganga Mkuu (W), Hospitali ya Wilaya Dkt. Paschal Mbota.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya - Kiteto (aliyeshika mfagio kushoto)
Watumishi wa Taasisi mbalimbali wakifanya usafi eneo la Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, Mjini Kibaya
............HABARI KAMILI.............
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto ndugu Tamim H. Kambona ameongoza watumishi kutoka taasisi mbalimbali za serikali kama vile Halmashauri, Magereza, Polisi , Mahakama na Takukuru kwenye zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika hospitali ya wilaya .Usafi huu umefanyika kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 03:00 asubuhi.
Zoezi hilo la kufanya usafi ni utekelezaji kwa vitendo wa maagizo ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. J.P.J. Magufuli kwamba katika kuazimisha siku hii muhimu kwa wanachi na Taifa letu, tufanywe usafi wa mazingira katika maeneo yote ya kutolea huduma za afya kote nchini.
Aidha katika utaratibu wa kawaida , zoezi la usafi wa Mazingira hufanyika kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi,ambapo wakazi wote wa wilaya hii ,walio watumishi na wasio watumishi hufanya usafi katika maeneo yao ya kazi,biashara na makazi .Na kwa mwezi Disemba zoezi hilo litafanyika tarehe 29.12.2018 kama tanzazo linavyoonyesha sehemu ya matangazo ya tovuti hii na katika mbao za matangazo ofisi za Serikali, Kata na Vijiji.
Baada ya zoezi la usafi ,watumishi walielekea katika uwanja mkuu wa michezo kwa ajili ya kushiriki kwenye Bonaza la watumishi,lililoandaliwa na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri chini ya usimamizi wa afisa michezo(W) na afisa utamaduni (W).
.................MWISHO....................
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa