• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

MHE. MWEMA AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO WANAOTEKELEZA MRADI WA JENGO MAALUMU LA KUJIFUNGULIA WANAWAKE NDOTOI

Imetumwa : December 18th, 2024

Mapema wiki hii  Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mheshimiwa Remidius Mwema amekutana  na kufanya mazungumzo na  Anna Walkowiak - Mwanzilishi & Mwenyekiti wa Bodi ya “Africa Help Foundation”  akiambatana na  Anna Paczkowska - Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake (Obstetrician - Gynecologist) kupitia mradi wao unaotekelezwa Wilayani Kiteto.


 Africa Help Foundation ni wadau wa maendeleo kutoka POLAND,  ambao wanatekeleza Mradi wa  Ujenzi wa Zahanati na Jengo maalum la kujifungulia wajawazito (Marternity Home) katika Kijiji cha Ndotoi, Kata ya Laiseri Tarafa ya Sunya.


Mradi huu unalenga kutoa huduma za afya hususani Afya ya Uzazi na Mtoto kwa jamii ya wafugaji na wananchi wote katika kijiji hicho ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga.


Aidha, mradi huo ni sehemu ya  kuunga mkono jitihada za serikali, kuhimiza jamii kuacha kujifungulia nyumbani na kwa wakunga wa jadi na badala yake jamii kuhamasishwa kutumia kituo hicho kupata huduma za afya pamoja na Elimu ya Afya kutoka kwa wataalam wanaoishi nao katika kijiji cha Ndotoi.


Mradi huu unatarajia kukamilika Januari ,2025 na wananchi  wa Ndotoi wameupokea kwa mwitikio chanya.

Hata hivyo, taasisi hiyo inakusudia kushirikiana na Serikali kuongeza huduma ya  uchunguzi wa vipimo mbalimbali kwa kujenga jengo la maabara.

Matarajio ya baadae ni kupandisha hadhi Kituo hiki kuwa kituo kamili cha Afya kwa kuongeza majengo ya Mama na Mtoto, chumba cha Upasuaji ili Huduma za upasuaji wa dharura na wa kupangwa kwa wajawazito wasioweza kujifungua kawaida ziweze kutolewa.


Ushirikiano baina ya Poland (Africa Help Foundation) na  Serikali ya Tanzania unalenga pia nyanja za kujengeana uwezo Wataalamu wa Afya kwa mafunzo (Training) na kubadilishana Wataalam/Watumishi (Staffs Exchange) kwa kutembeleana Muda flani katika nchi hizi mbili.


Serikali itaendelea Kupeleka Watumishi,Madawa,Vitendanishi,Vifaa na vifaa tiba na kukisimamia kituo kwa uendelevu kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya hapa nchini ili kituo hiki kiweze kutoa huduma bora  za Afya kwa Wananchi wa Ndotoi.

Aidha, Serikali inatambua, inathamini na kuheshimu  mahusiano mema  na Wadau wote wa Maendeleo ikiwa ni pamoja na  Africa Help Foundation.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa