Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti Akizungumza na Wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Asubuhi ya Tarehe 10.09.2020 (picha maktaba)
------------------------------------------- HABARI KAMILI -------------------------------------------
Mh. Mkuu wa Mkoa huyo alifika wilayani Kiteto tarehe 10.09.2020 kwa shuguli za kikazi ya siku moja ambapo aliongea na wafanyakazi katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kisha kutoa maagizo ya "kutofanya kazi kwa mazoea na kujitahidi kutumia weledi na kushirikiana na wenzako siku zote".
Mh. Mkuu wa Mkoa Joseph Mkirikiti alisema " huko nje kwa kipindi cha nyuma Kiteto ilikuwa inajulikana kama wilaya ya migogoro ya wakulima na wafugaji lakini migogoro hiyo japo kwa kiasi kikubwa imepungua sana lakini bado tunatakiwa tutumie wataalamu waliopo ili kupunguza kero hizi na hatimaye kutokomeza kabisa hali hiyo kutijirudia tena"
Aidha kuhusiana na wafanyakazi kuwa wachache katika kila idara na vitengo katika halmashauri, Mh. Mkuu wa Mkoa huyo alisema " ni muhimu sana kuwa wazalendo kwani mtaalamu aliyepo katika halmashauri makao makuu hapa awatumie Maafisa Tarafa, Maafisa Watendaji wa Kata na Maafisa Watendaji wa Vijiji kwani wao wana watumishi wengi watafanya hizo kazi kwa muda mfupi na kupata majibu ya haraka."
Dhana ya ugunduzi, ubunifu na ushirikiano wa kikoa ni muhimu sana katika kazi ili kufanikisha majukumu yetu mbalimbali ya kuwasaidia wananchi lakini tukiwekeana vikwazo sisi kama watumishi, kwa kila mtu kujiona yeye ni bosi basi kila kitu tunachokipanga hakitafanikiwa.
Hata hivyo Mh. Mkuu wa Mkoa huyo Joseph Mkirikiti aliendelea kwa kusema "Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mh. Rais Dkt. J.P.Magufuli imefanya kazi kubwa sana kwa muda mfupi wa miaka hii 5 kuanzia sekta ya Afya katika ujenzi wa Hospitali na vituo vya Afya nchi nzima, sekta ya miundombinu ujenzi wa reli ya kimataifa, barabara, madaraja, vivuko na upanuzi wa viwanja vya ndege, sekta ya anga ununuzi wa ndege, sekta ya nishati ujenzi wa mradi mkubwa wa ufuaji wa umeme wa Nyerere hydro electric power, usimamiaji mzuri wa sekta ya madini na utalii yote haya yameifanya nchi kupaa hadi kuingia uchumi wa kati". Sasa hivi mtu anatoka Mkoa wa Mtwara hadi Mkoa wa Kagera - Bukoba kwa gari ndogo akiwa kwenye barabara ya lami kitu ambacho huko nyuma haikuwa hivyo, kwa hiyo nasisi tumuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii Mh. Rais Dkt J. P. Magufuli ili tupate mafanikio makubwa zaidi.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa