Katika mwaka wa Fedha 2023/2024, mfuko wa Jimbo la Kiteto litatoa kiasi cha fedha 92,297,000 ikiwa ni mchango kwaajili ya miradi ya maendeleo katika kata 12 jimboni hapo.
Hayo yamebainishwa Desemba 28,2023 katika kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo ambacho kiliongozwa na Mbunge wa Jimbo la Kiteto, Mh. Edward Olelekaita.
Katika sekta ya Elimu, Mfuko wa jimbo utachangia jumla ya shilingi 44m katika ukamilishaji wa vyumba nane vya madarasa, utengenezaji wa madawati na ukamilishaji wa nyumba mbili za za walimu.
Upande wa sekta ya afya Mfuko wa Jimbo utachangia jumla kiasi cha shilingi 12,584,000 katika ukamilishaji wa nyumba mbili za madaktari.
Aidha Mfuko wa Jimbo utachangia kiasi cha shilingi 10m katika ukamilishaji wa soko la Kijiji cha Sunga.
Mbali na miradi hiyo, Mfuko wa Jimbo utachangia mifuko ya sementi yenye julma ya thamni ya shilingi 20,713,000.
Vilevile Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Olelekaita, alimuagiza Katibu wa Kamati Ndugu Erasmo Tellun Ndelwa, kuandaa ziara ya wajumbe wa kamati hiyo ili kwenda kukagua miradi iliyochangiwa fedha katika mwaka wa fedha 2021/2022 na 2022/2023 ili kujiridhisha endapo pesa za mfuko wa jimbo zinafanya kazi zilizokusudiwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa