Watumishi wa serikali kuu na serikali za mitaa wakishindana kuvuta kamba wakati wa bonanza lililofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania bara.Bonanza hilo limefanyika katika uwanja mkuu wa michezo Kibaya mjini.
Watumishi wakishindana kunywa soda na mkate mzima.
Baadhi ya watumishi wakishindana kukuna nazi .
Watumishi wakicheza draft
............HABARI KAMILI...........
Watumishi kutoka idara mbalimbali za serikali na taasisi binafsi wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara wameungana na Watanzania wengine katika kuadhimisha miaka 57 ya uhuru wa Tanzania bara kwa Bonanza la watumishi. Bonanza hilo limefanyika Jumapili tarehe 09/12 /2018 kwenye uwanja mkuu wa michezo uliopo katika mji mdogo wa Kibaya.
Akizungumza wakati akifunga Bonanza hilo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Mgeni rasmi bi Dhulfa P. Laizer ambaye pia ni Afisa tarafa ya Kibaya amesema‘‘ Michezo hii ilikuwa ni mashindano , kwenye mashindano huwa kuna washindi na walioshindwa. Ambao hamkushinda mna nafasi ya kujipanga upya,ili wakati mwingine tutakapokuwa na Bonanza kama hili,mshinde’'.
Kadhalika bi Laizer amesema kwamba ingawa kuna waliopata ushindi,lakini yeye kwa upande wake kwa jinsi alivyotazama wakati michezo yote inachezwa, ameona kwamba washiriki wote wamejitahidi kucheza vizuri.Aidha amewashukuru sana kwa bidii na moyo wa kujituma waliouonyesha katika michezo yote.
Washindi wa michezo hiyo wamepewa zawadi mbalimbali .Sambamba na zawadi hizo Bi Laizer amewapongeza washiriki wote kwa kushiriki michezo hiyo, kwani kupitia ushiriki wao ,wameifanya siku hiyo kuwa ya kipekee na ya furaha sana.
Katika Bonaza hilo kulikuwa na michezo mbalimbali , michezo hiyo ni Mpira wa miguu, mpira pete,kukimbiza kuku ,kuvuta kamba,bao,draft, kukuna nazi,kunywa soda kwa wanawake,kunywa soda na mkate mzima kwa wanaume, pamoja na kukimbia ndani ya magunia.
..........MWISHO...........
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa