Kitengo cha Lishe katika wilaya Kiteto kimetoa mafunzo maalum kwa walimu 64 kutoka katika shule za sekondari 9 na msingi 55. Mafunzo hayo yamefanyika kwa lengo la kuongeza uelewa na maarifa ya walimu kuhusu lishe bora kwa wanafunzi na uanzishwaji wa bustani za mboga mboga kwa lengo la kuboresha afya na maendeleo ya watoto shuleni.
Hayo yamebainishwa na kwenye taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kitengo hicho kwenye Robo ya Kwanza ya mwaka 2024/25 kwenye kikao cha Kamati ya Lishe kilichofanyika Oktoba 25,2024.
Katika mafunzo haya, walimu wamefundishwa juu ya umuhimu wa lishe bora, uundaji wa klabu za lishe shuleni na muongozo wa utoaji wa vyakula shuleni. Baada ya mafunzo hayo, waalimu hao walipewa jukumu la kuanzisha club za lishe shuleni, ambapo wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu lishe bora na kuanzisha bustani za mbogamboga na matunda.
Afisa Lishe wa Wilaya, Beatrice Lutanjuka. amesema kuwa mafunzo hayo ni hatua muhimu katika kupambana na tatizo la utapiamlo na kuimarisha afya ya wanafunzi, ambao ni sehemu ya baadaye ya taifa. Aliongeza kuwa klabu za lishe zitasaidia kubadilisha mitazamo ya wanafunzi kuhusu ulaji bora na kuwa na maisha yenye afya bora.
*Wanafunzi watakaojiunga na klabu hizi watapata fursa ya kushiriki katika shughuli mbalimbali kama vile bustani za shule za mboga na matunda, mashindano ya upishi wa vyakula bora, na kampeni za lishe ndani na nje ya shule. Mafanikio ya mpango huu yanategemewa kuleta mabadiliko chanya kwa afya na maendeleo ya watoto katika jamii.*
Kwa nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhe. Remidius Mwema na Mkurugenzi Mtendaji (W) CPA. Hawa Abdul Hassan, wamekipongeza Kitengo cha Lishe kuwezesha kuanzisha klabu za lishe shuleni.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa