• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KINNAPA YAKABIDHI MRADI WA UFUNDI SHULE YA SEKONDARI SUNYA

Imetumwa : August 1st, 2024

Shirika lisilo la kiserikali KINNAPA limekadhi Mradi wa Ufundi Ushonaji kwa  Sekondari ya Sunya ili kuuendesha.

Hafla ya makabidhiano ya mradi huo imefanyika Julai 31,2024,  katika Shule ya Sekondari Sunya na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi, viongozi wa Chama na serikali na wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Kiteto. Mgeni Rasmi wa hafla hiyo alikua Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema.

KINNAPA imekua ikifanya jitihada ya kuwasaidia  wanafunzi waliokatisha masomo kurudi shuleni ili kuendelea na masomo ila ilikuja kubaini kua sio wanafunzi wote wapo tayari kurudi shuleni kuendelea na masomo ya kawaida darasani bali wapo ambao wanahitaji kujifunza ufundi.

Baada ya kutambua hilo, KINNAPA iliamua kuongeza mkondo wa ufundi katika shule ya Sekondari Sunya ili kuwapa fursa  wanafunzi waliokatiza masomo kupata ujuzi.

Mradi huo wa ufundi umegharimu kiasi cha fedha 5,100,000 ambayo imetumika kununua mashine(cherehani) mbalimbali tano ikiwemo mashine za kushonea na kudarizi, kununua vifaa vyote vya ushonaji, kununua majora ya vitambaa vya sare za shule ambayo yanatumika kama mtaji wa kuwezesha kuendeleza mradi huo. Aidha sehemu ya fedha hizo ilitumika kuwasaidia nauli wanafunzi wa darasa hilo la ufundi.

Mbali na hayo, KINNAPA pia imesaidia upatikanaji wa mwalimu wa ufundi kwa darasa hilo ambapo uongozi wa shule unapaswa kuwajibika kumlipa mwalimu huyo mshahara. Hii imepelekea Mkuu wa Wilaya Mhe. Mwema kutoa kiasi cha fedha 300,000 ili kuisaidia shule hiyo mshahara wa mwalimu huyo na pia shirika la SULEDO limeahidi kutoa pia 300,000 lengo hilohilo. 

Mradi huo ambao kwa sasa una wanafunzi 13, umekadhibiwa kwa Mkuu wa Sekondari ya Sunya ili kuuendesha na mafunzo hayatatolewa kwa wanafunzi waliokatiza tu masomo  bali hata kwa wanafunzi wengine  watakaohitaji kupata ujuzi  huo.

Akijibu swali ambalo liliuliza kwanini mradi huo umetekelezwa Sunya na sio kwenye kata nyingine, Mratibu wa KINNAPA Kiteto Ndg. Abrahamu AKilimali, amesema kwamba Sunya ndio walianza kuonesha  muitikio wa kuwarudisha shuleni  wanafunzi waliokatisha masomo na vilevile Sunya ina idadi kubwa ya watoto waliorudi kuendelea na masomo baada ya kukatisha masomo kwa sababu mbalimbali.





Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa