Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mhe. Remidius Mwema, amewaagiza Watendaji wa Kata katika Halmashauri hiyo kupita kwenye shule zote zilizopo kwenye kata zao ili kufanya ukaguzi wa chakula kwaajili ya wanafunzi.
Maagizo hayo yametolewa Agosti 1, 2024 katika Ukumbi wa Halmashauri katika Kikao cha Tathmini ya Mkataba wa Lishe wilayani hapo.
Mhe. Mwema amewaagiza watendaji hao kupita kwenye kila shule kwenda kufanya tathmini ya mavuno yaliyopatikana kama yatatosha kwaajili ya chakula cha wanafunzi mpaka kwenye msimu ujao wa mavuno na endapo kutakua na upungufu wajue mikakati ya kukabiliana na upungufu huo.
“Mbali na kufanya tathmini ya uwepo wa chakula nawaagiza mkienda huko muangalie pia uhifadhi wa chakula upoje ili mjionee kama chakula kinahifadhiwa kwa kufuata kanuni za uhifadhi na pia mfuatilie kama kuna wizi wa chakula na endapo mtabaini kuna wizi hatua zichukuliwe”, ameongeza Mhe. Mwema.
Aidha Mhe. Mwema amewaagiza Watendaji hao kuweka wazi taarifa za mavuno kwa wazazi. “Itisheni vikao vya wazazi mseme kwenye mashamba ya shule mavuno yaliyopatikana ni kiasi gani halafu mseme kuna upungufu wa kiasi gani ili mzazi ajue nini kimepatikana na yeye anawajibika kutoa kiasi gani cha chakula ili kuwezesha mtoto wake kula chakula shuleni mwaka mzima”,ameongeza Mhe. Mwema.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa