Mwenyekiti wa Kamati ya Lishe Bw. Emmanueli Mwagala Akifungua Kikao cha Kamati ya Lishe kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Tarehe 22.10.2019 Katika Ukumbi wa Halmashauri.
Wajumbe Mbalimbali Katika Kikao cha Kamati ya Lishe Wakisikiliza Mada.
Kisha uwasilishaji wa taarifa mbalimbali za Utekelezaji Majikumu ya Lishe kwa Kipindi cha Robo Mwaka ya Kwanza (Juali 1 hadi Septemba 30 2019) ulianza kwa Idara na Vitengo kama unavyojionea hapo chini.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Beatrice Lutanjuka Akiwasilisha Taarifa.
Bi. Nathalia Gwacha Akiwasilisha Taarifa ya Kitengo cha Uzazi, Mama na Mtoto toka Hospitali ya Wilaya ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmshauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Jackline Balongo Akifafanua Miongozo Mbalimbali ya Jamii iliyogawanyika Katika Vitengo Vikuu Vitatu navyo ni:-
Kitengo cha huduma ya ustawi wa familia na watoto; malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo,
Kitengo cha marekebisho ya tabia na haki za mtoto,
kitengo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee
Bw. Seleman Andrew Akiwasilisha Taarifa kwa Niaba ya Wafanya Biashara Wa Mashine za Kukamua Mafuata ya Alizeti Wilayani Kiteto.
Bw. Ibrahim Bory Akiwasilisha Taarifa kwa Niaba ya BAKWATA Wilayani Kiteto.
Bw. Pundugu Balabala (Kaimu Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika Wilaya) Akiwasilisha Taarifa .
Wakatikati ni Bw. Lucas Mgubika (Kaimu Afisa Afya na Mazingira Wilaya) Akiwasilisha Taarifa na Kutoa Ufafanuzi Katika Baadhi ya Maeneo Aliyoyawasilisha .
Kutoka Kushoto Bw. Japhet Malya (Kaimu Afisa Maeneleo ya Jamii Wilaya) Akiwasilisha Taarifa na Kutoa Ufafanuzi Katika Baadhi ya Maeneo Aliyoyawasilisha .
Katikati Bw. Birikaa Olesikilal (Kaimu Afisa MMifugo na Uvuvi Wilaya) Akiwasilisha Taarifa na Kutoa Ufafanuzi Katika Baadhi ya Maeneo Aliyoyawasilisha .
Kulia ni Bw. Temba Mfamasia wa Wilaya akiwasilisha Taarifa na Kutoa Ufafanuzi Katika Baadhi ya Maeneo Aliyoyawasilisha.
Bw. Fabian Simon Kaimu Afisa Elimu Sekondali wa Wilaya akiwasilisha Taarifa na Kutoa Ufafanuzi Katika Baadhi ya Maeneo Aliyoyawasilisha.
---------------------------------------------- HABARI KAMILI ----------------------------------------------
Walaji wa Samaki Mjini Kibaya na Vijijini wapelekea kuongezeka kwa wafugaji wa samaki Wilayani Kiteto; hayo yamejiri kwenye kikao cha Kamati ya Lishe Wilaya ya Kiteto ambacho ni kikao cha robo ya kwanza ya mwaka tarehe 22.10.2019 kuhusu utekelezaji wa kazi mbalimbali za Lishe katika sekta tofauti kuanzia Julai - Septemba 2019. Katika kikao hicho imefahamika kwamba miaka 20 iliyopita kulikuwa na samaki wanaotokana na mabwawa ya asili ambayo ni machache kama vile bwawa la Namelock Kata ya Namelock. Wananchi wa maeneo husika wamekuwa wakivua samaki hizo kwa lengo la kupata kitoweo lakini baada ya watu kuongezeka na muingiliano wa jamii mbalimbali hapa Kiteto imepelekea kutotoshereza mahitaji ya soko la ndani hii imepelekea wachuuzi kununua samaki toka nje ya Wilaya kwa wingi na wengine kuanza kufuga kwa mabwawa ya kisasa ya nyumbani hapa Kiteto.
Baadhi ya wananchi ambao wanajulikana hadi sasa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kupitia Idara ya Mifugo na Uvuvi wanafuga samaki hao ni watano (5) kwa majina ni Mzee Omary Mohamedi wa Kata ya Matui ambao ni mji wenye watu wengi, Mzee Puputo wa Kata ya Sunya, Mzee Khalifa Selemani wa Kata ya Kiperesa, Askofu wa Kanisa la Anglikana Kibaya Bwana Isaya Chambala na wa mwisho ni Mwalimu Mchomvu wa Kibaya Mjini.
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiria mali wote katika fursa mbalimbali ikiwemo hii ya ufugaji wa samaki kwa kuhamasisha wananchi wafuge kwa wingi kwani soko lipo kubwa lakini pia kutumia wataalamu wa mifugo waliopo ili kuongeza tija ya uzalishaji wa samaki hao itakayopelekea uboreshaji wa lishe za wananchi. Faida iliyopo kwa wafugaji wa ndani ni kutumia wataalamu wa Halmashauri na kwa wananchi watapata kitoweo cha samaki kwa bei nafuu zaidi ukilinganisha na samaki zinazotoka mikoani, lakini ikumbukwe kuwa ajira elekezi za kisekta huchipuka kutokana na shughuli hizi za ufugaji wa samaki.
Hata hivyo wadau wa Kamati hii ya Lishe Wilayani Kiteto wameipongeza sana Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa kusimamia upandishaji holela wa bei ya nyama Wilayani Kiteto ambapo ilipaa hadi kufikia shilingi za kitanzania 7000/= kwa kilo moja ikiwa ni ongezeko la Shilingi za Kitanzania 1000/= sawa na asilimia 16.66%. Kupongezwa huku kunamaanisha Serikali inafanya kazi nzuri ya kuwasikiliza wananchi bila kubagua walio nacho na wasionacho ambapo matokeo yake ni kupatikana kwa lishe bora katika familia nyingi kwa maamuzi haya. Lishe inapokuwa ni bora rika mbalimbali la binadamu hunufaika vilivyo kutokana na upatikanaji wa protini ya kutosha inayojenga mwili na madini mbalimbali kwa mwili wa binadamu kwa mujibu wa wataalamu wa lishe.
Suala la kuboresha miundombinu ya machinjio liko pale pale na linasimamiwa lakini kasi zaidi itakuwepo ya kubadilisha miundombinu iliyopo ili iwe kubwa na ya kisasa zaidi kulingana na upatikanaji wa fedha za utekelezaji miradi husika kutoka Halmashauri.
Kuhusiana na Idara ya Ustawi wa Jamii katika Halmashauri zote nchini ina vitengo vitatu (3) vyenye majukumu yafuatayo yanayofanya kazi kwa kuzingatia sera, miongozo, kanuni na sheria za Nchi;kitengo cha kwanza ni Kitengo cha huduma ya ustawi wa familia na watoto; malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto wadogo kwa mujibu wa sheria ya Ndoa Na. 5 ya mwaka 1971; Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009;sheria ya kuzuia usafirishaji Haramu wa binadamu "the Ant-trafficking in Persons" Act, 2008
Kitengo cha pili ni Kitengo cha marekebisho ya tabia na haki za mtoto kisheria kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009, sheria ya huduma za majaribio na ujenzi wa tabia, sheria ya makosa ya kujamiiana Na 4 ya mwaka 1998, sheria ya kanuni za adhabu na sheria ya huduma kwa jamii Na.6 ya Mwaka 2002
Kitengo cha tatu ni kitengo cha huduma kwa watu wenye ulemavu na wazee kwa mujibu wa sera ya taifa ya wazee;sera ya taifa ya maendeleo na huduma kwa watu wenye ulemavu (2004); kwa mujibu wa sheria ya watu wenye ulemavu Na 9 ya 2010.Hivyo milango iko wazi kwa wananchi wote kufika Ofisi za Halmashauri ili kuweza kupata msaada wa kisheria katika changamoto zinazohusu makundi husika.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa