Katika kikao cha Kamati ya fedha na mipango cha tarehe 11/3/21 Halmashauri ya wilaya ya kiteto kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ambapo kiliongozwa Mwenyekiti wa halmashauri Mhe .Abdala Bundala. Wajumbe wa kamati hiyo kwa pamoja walipitisha vyazo vipya vya mapato vilivyowasilishwa na uongozi wa halmashauri ilikuweza kuongeza mapato ya halmashauri .
vyanzo hivyo vipya vya mapato vilvyopitishwa na kamati hiyo ni tozo katika mashamba makubwa na matrekta kwa msimu
kama vifuatazo:
1. Ekari 50 Tsh.100, 000/= kwa msimu
2. Ekari 51-100 Tsh.150, 000/= kwa msimu
3. Ekari 101-200 Tsh.200, 000/= kwa msimu
4. Ekari 201-500 Tsh.500, 000/= kwa msimu
5. Trekta kiwango cha tozo ni Tsh.50, 000/= kwa msimu
Tozo hizi zitaanza kutozwa mwaka ujao wa fedha 2021/2022
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa