• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC Ataka Suala la Lishe Kuwa Kipaumbele

Imetumwa : December 5th, 2018
  1. Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magesa akifungua kikao kazi cha mafunzo ya awali ya mipango ya bajeti ya masuala ya lishe ngazi ya halmashauri. Waliokaa kushoto ni kaimu Katibu Tawala ( W)  Ndg. Fadhili Alexander, kulia ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya wilaya ya Kiteto Ndg. Zabron Lulandala.



.......HABARI KAMILI..........




Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mhe. Tumaini Magessa  amewataka wakuu wa idara za Halmashauri ya wilaya ya Kiteto zinazohusika na shughuli za lishe kuweka kipaumbele katika suala la lishe, ili kuiepusha jamii na na udumavu. Mhe. Magessa ameyasema hayo wakati akifungua kikao kazi cha mafunzo ya awali ya mipango na bajeti ya masuala ya lishe ngazi ya Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa hospitali ya wilaya  mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mheshimiwa Magessa amesema“ tatizo la lishe linasababisha udumavu wa mwili na akili,pia linasababisha kuongezeka kwa magonjwa yasioambukiza yanayotokana na ukosefu wa chakula bora pamoja na ulaji mbaya usiozingatia misingi ya afya bora.Katika tatizo la lishe duni,hali ni mbaya zaidi kwa watoto ,kina mama wajawazito  na wanaonyonyesha.Watoto wadogo ndio waathirika zaidi wa matatizo yanayotokana na lishe duni’’.

Mhe . Magessa amesema kwamba suala la lishe,linatakiwa kupewa kipaumbele na watu wote,kwa sababu suala hilo bado ni tatizo katika  jami,jamii bado inauelewa mdogo kuhusu mlo kamili.Hali ya kuwa Ustawi wa jamii unategemea hali nzuri  ya lishe.Kama lishe ni duni jamii haiwezi kuwa na ustawi mzuri , kwa sababu hata uwezo wa kufikiri wa watu utakuwa mdogo.


Kadhalika Mheshimiwa Magessa ameeleza matarajio yake kwa wakuu hao wa idara  baada ya mafunzo hayo ambapo amesema kwamba anatarajia kuwa kikao kazi hicho kitakuwa na tija , lakini ni lazima  mipango yote   waliyonayo kuhusu masuala ya lishe waiweke kwenye utekelezaji, na  wahakikishe kuwa mipango hiyo inaigusa jamii. Amewataka kuweka kumbukumbu na takwimu kwa yale yote wanayotekeleza, kwani kwa kufanya hivyo, itawapa wepesi wa kufahamu ni yapi yametekelezwa, yametekelezwa kwa kiwango gani ,na yapi ambayo hayajatekelezwa.

Pia Mheshimiwa Magessa amesema kwamba vikao hivyo ni muhimu sana katika kujifunza ,kwa kuhudhuria katika vikao hivyo mtu anapata kitu ambacho kina mpa ari ya kutafiti zaidi.Anapokwenda kutafiti anajifunza vitu vingi zaidi.Vilevile Mhe. Magessa amesema kwamba wilaya imeazimia kufanya mapinduzi ya kilimo kwa lengo la kulima kilimo chenye tija kitakachoboresha kipato cha wananchi sambamba na kuboresha lishe,hivyo kikao hicho ni cha muhimu kwa sababu yale yatakayoazimiwa, yatakwenda kufanyiwa kazi.

Aidha Mhe. Magessa amesema kwamba ni muhimu kwa Mwenyekiti wa Halmashauri kuwashirikisha madiwani maazimio yote ya vikao hivyo kwani madiwani ndio kiungo muhumu cha  kupeleka taarifa kwa wananchi kwenye kata zao.

Kikao kazi hicho cha siku moja kimehitimishwa kwa majadiliano ambapo kila mkuu wa idara alieleza ni kwa namna gani idara yake inatekeleza shughuli za lishe.



........MWISHO.............

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI SEPTEMBA 2023 September 03, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TABIA MBAYA ZA WATUMUSHI ZINAHARIBU SIFA ZA TAASISI

    May 01, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI KITETO LIMEMPONGEZA RAIS SAMIA.

    May 30, 2025
  • PONGEZI KWA WANANCHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

    April 28, 2025
  • TUUENZI MUUNGANO WETU

    April 27, 2025
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa