• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe watumishi |
    • Malalamiko |
Kiteto District Council
Kiteto District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Idara
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Afya
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
      • Sheria
      • Teknolojia,Habari ,Mawasiliano na Mahusiano
      • Nyuki
    • Muundo wa Halmashauri
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Uchimbaji Madini
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za afya
    • Huduma za elimu
    • Huduma za Maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Ardhi na Maliasili
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • This page is under construction
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na uongozi
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi,Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi mipya
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa wateja
    • Mpango mkakati
    • Taarifa mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Ardhi na Maliasili

  • UTANGULIZI
  • Idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ni miongoni mwa idara zinzounda Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto. Idara hii imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni sekta ya ardhi na sekta ya maliasili. Sekta ya Ardh ina sehemu nne ambazo ni ardhi, Upimaji na ramani, Mipangomiji na Vijiji na sehemu ya uthamini.  Sekta ya Maliasili ina sehemu tatu ambazo ni misitu, wanyamapori, mazingira. Majukumu makuu ya idara ni kama ifuatavyo;
  • Kuratibu na kusimamia masuala yote yanayohusu ardhi ikwepo upangaji wa maeneo, upimaji wa viwanja na mashamba, uthamini wa ardhi na mali zisizohamishika, uchoraji wa ramani na kusimamia uendelezaji wa miji na mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi Na.4 ya 1999, Sheria ya Ardhi Na.5 ya 1999, Sheria ya Mipangomiji Na.7 ya 2007 na sheria nyinginezo za nchi.
  • Kulinda, kusimamia uendelezaji na uhifadhi ya misitu ya jamii kwa njia shirikishi.
  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria za Misitu Na.14 ya 2002 na Kanuni zake.
  • Kusimamia uvuanaji endelevu wa mazao ya misitu.
  • Kusimamia na kuratibu shughuli za wanyamapori ikiwepo shughuli za uwindaji na utalii.

 

    2.0 Idadi ya Viwanja

Halmashauri ya wilaya ya Kiteto ina jumla ya viwanja 5,574 vilivyopimwa ambapo viwanja 4,631 vimefanyiwa upimaji wa awali na 963 upimaji wake umekamilika na ramani kuidhinishwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mchanganuo wa viwanja hivyo ni kama inavyoonekana kwenye jedwali namba 1.

Jedwali na 1. Taarifa ya viwanja katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto.

S/NA

KITALU

ENEO

IDADI YA VIWANJA

VIWANJA VYA DEMARCATION

VIWANJA VILIVYOKAMILIKA UPIMAJI

1
A
Kibaya Mjini
130
NIL
130
2
B
Bomani
467
252
215
3
C
Kibaya Mjini
455
125
330
4
D
Mafichoni
452
441
11
5
E
Kibaya Mjini
810
805
5
6
F
Kibaya Mjini
762
757
5
7
G
Kibaya Mjini
998
785
213
8
H
Kibaya Mjini
93
93
Nil
9
I
Kibaya Mjini
10
6
4
10
A
Sunya
33
33
Nil
11
B
Sunya
38
38
Nil
12
C
Sunya
3
3
Nil
13
A
Matui
400
400
Nil
14
B
Matui
454
454
Nil
15
C
Matui
218
201
17
16
A
Engusero
38
38
Nil
17
B
Engusero
41
41
Nil
18
C
Engusero
3
nil
3
19
A
Njoro
44
44
Nil
20
B
Njoro
40
40
Nil
21
A
Partimbo
35
35
Nil
22
B
Partimbo
40
40
Nil
23
C
Partimbo
10
nil
10
 
 
JUMLA
5574
4631
943

Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi (W) Kiteto, 2018

3.0   Upimaji wa Mashamba na utoaji Hati miliki za Kimila

Halmashauri katika kipindi cha kuanzia 2013 hadi sasa imepima jumla ya mashamba 3,124 katika vijiji vya Mbigiri, Chapakazi, Namelock, Ndaleta, Partimbo, Kimana na Loltepes na kutoa hati miliki za kimila 1,205.  Katika vijiji vya Namelock, Kimana na Loltepes utoaji wa hati miliki za kimila bado haujafanyika kwa Tume ya Matumizi bora ya Ardhi imeelekeza kufanya marekebisho ya mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji hivi. Hati za kimila zilizotolewa katika vijiji vya Namelock na Kimana zilitolewa kabla ya tume ya matumizi bora ya ardhi kuja kushirikiana na wataalamu wa PLUM team ya wilaya kupima mashamba. Mchanganuo wa upimaji wa mashamba na utoaji hati miliki umeonyeshwa kwenye jedwali namba 2.

Jedwali Na. 2: Upimaji mashamba na utoaji Hati Miliki za Kimila

S/NA
KIJIJI
IDADI YA MASHAMBA YALIYOPIMWA 
IDADI YA MASHAMBA YALIYOPIMWA NA KUANDALIWA HATI
1
Mbigiri
921
921
2
Chapakazi
248
248
3
Namelock
404
10
4
Ndaleta
4
4
5
Partimbo
26
26
6
Kimana
1,144
3
7
Loltepes
384
0
8
Amei
186
0
9
Ngabolo
26
26
10
Ndedo
25
25
11
Olkitikiti
1
1
12
Dosidosi
2
2
 
Jumla Kuu
3371
1,266

Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi (W) Kiteto, 2018

 

4.0. Mashamba Makubwa

Halmashauri ina jumla ya mashamba 9 yenye Hati Miliki (Certificate of occupancy) katika vijiji vya Namelock, Ndaleta, Partimbo na Kimanakama yanavyoonekana katika jedwali namba 6. Aidha halmashauri ina jumla ya mashamba 2 yenye offer (registered letter of offer of right of occupancy) katika vijiji vya Kimana na Magungu kama inavyoonyeshwa kwenye jedwali Na 3.

Jedwali na 3: Mashamba yenye Hati (Certificate of Occupancy)

NA

KIJIJI

SHAMBA NAMBA

MMILIKI

ANUANI

HATI NAMBA

TANGU 

UKUBWA

MATUMIZI

MUDA

1

KIMANA

559

Benedict Kiroia Loosurutia
BOX 34 KIBAYA
OFFER
1/4/1993
1235 Eka
Agriculture Purposes
   33 YRS

2

Namelock

2666 & 2667

KITETO AGRO BUSSINES LTD

BOX 2887 DODOMA
28718

17/5/2010

141.51 Ha

Agriculture & pastoral    use Group 'R' use classes  (c) &(b)

33 YRS

3

Namelock

2664 & 2665

KITETO AGRO BUSSINES LTD

BOX 2887 DODOMA
28719

17/5/2010

112.58 Ha

Agriculture & pastoral    use Group 'R' use classes (c) &(b)

33 yrs

4

Namelock

2668 & 2669

KITETO AGRO BUSSINES LTD

BOX 2887 DODOMA
28723

17/5/2010

144 Ha

Agriculture & pastoral    use Group 'R' use classes  (c) &(b)

33 YRS

5

Namelock

2670

KITETO AGRO BUSSINES LTD

BOX 2887 DODOMA
28717

17/5/2010

60.29 Ha

Agriculture & pastoral    use Group 'R' use classes  (c) &(b)
33 Yrs

6

Namelock

2752

NDININI SABAYA SIKAR

BOX 15240 ARUSHA
35865

13/4/2012

39.11 Ha

Plant & Animal husbandry    use Group 'R' use classes (c) &(b)

33 yrs

7

Namelock

2753

NDININI SABAYA SIKAR

BOX 15240 ARUSHA
35866

13/4/2012

32.98 Ha

Plant & Animal husbandry    use Group 'R' use classes (c) &(b)

33 yrs

8

Magungu

2267/1-2267/5

ARUSHA CO-OPERATIVE UNION LTD (ACU)

BOX 7073 ARUSHA
OFFER

19/7/1989

2706 Eka

Plant & Animal husbandry    use Group 'R' use classes (a) (b) &   ©

99 yrs

9

Partimbo

3079

Wiliam Elisikia Msuya

Box.42 Kibaya
42263
  6/3/2014
16.9 Eka
Plant & Animal husbandry    use Group 'R' use classes (c) (b) &  ©

33 yrs

10

Ndaleta

2725

Fegro Farm LTD

BOX 71411 DSM
39829

29/4/2013

443,258     Sqm
Plant & Animal husbandry    use Group 'R' use classes (c)

33 YRS

11

Partimbo

3059 & 3060

Gabriel Simon Kishapwe
Box.48 Kibaya
40780

7/10/2013

 

72 Eka

Plant & Animal husbandry    use Group 'R' use classes (c)

33 yrs












 

Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W), Kiteto 2018

5.0    Michoro ya Mipango Miji

Halmashauri imefanikiwa kuandaa michoro ya mipango miji 15 yenye jumla ya viwanja 7,015 vya matumizi mbalimbali katika mji mdogo wa Kibaya. Michoro mingi ya maeneo haya imeandaliwa baada ya maeneo hayo kuwa tayari yameshajengwa na wananchi, hii ni kutokana na kutokuwa na Mtaalamu wa Mipango Miji na Vijiji.

Jedwali na. 4 michoro ya mipango miji ambayo imeidhinishwa na mkurugenzi wa mipango miji.

S/N
NAMBA YA MCHORO
JINA LA MCHORO
IDADI YA VIWANJA
1
21/KBY/01/102010
Bomani layout plan

421

2
21/KBY/01/102010A
Amendment of Bomani lay out plan

76

3
21/KBY/01/102010B
Extension of Bomani lay out plan

161

4
21/KBY/02/102010
Majengo Mapya lay out plan

998

5
21/KBY/03/062010
Squatter upgrading of Mafichoni area

420

6
21/KBY/03/062010A
Extension of squatter upgrading of Mafichoni area

64

7
21/KBY/04/092011
Squatter upgrading of Kaloleni area phase -I

650

8
21/KBY/05/092011
Squatter upgrading of Kaloleni area phase -II

254

9
21/KBY/06/032012
Amendment of TP no. 21/Kby/03/062010 and gap filling

750

10
21/KBY/08/032012
Laalakir area

50

11
21/KBY/09/122012
Squatter upgrading of Magubike area

960

12
21/KBY/01/032012
Squatter upgrading of Engusero area

650

13
21/KBY/01/032012
Squatter upgrading of Matui area

231

13
21/KBY/01/042014
Lay out plan of Nasetani area

423

14
21/KBY/10/062014
Lay out plan of Laalakir area

316

15
21/KBY/13/102015
Layout plan of Msakasaka /Msente area

591

 
JUMLA KUU

7015

Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji 2018

6.0 Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya, Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji na Kata

Wilaya ilifanikiwa kuzindua Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya tarehe 6/6/2016 na linafanya kazi ipasavyo. Changamoto yake ni kwamba Mwenyekiti wa Baraza huhudumia pia Wilaya za Simanjiro na Kilindi, hali hii inamnyima muda wa kutosha kushughulikia migogoro iliyo mingi katika Wilaya hii. Aidha, tunayo Mabaraza ya ardhi katika ngazi ya Kata na vijiji ambapo Halmashauri imefanikiwa kuanzisha mabaraza 23 ya Kata kati ya kata 23 zilizopo na mabaraza 45 ya vijiji kati ya vijiji 63 vilivyopo. Kati ya vijiji 63 vya wilaya ya Kiteto, vijiji 19 vina masjala ya ardhi ya vijiji na vijiji vingine vikiwa katika harakati mbalimbali za ujenzi wa masjala ya ardhi ya vijiji vyao.

 

Jedwali na.6: Mabaraza ya ardhi ya vijiji na kata 

 

S/N
IDADI YA KATA
MABARAZA YA KATA
UPUNGUFU
IDADI  YA VIJIJI
MABARAZA YA ARDHI YA VIJIJI
UPUNGUFU
1
23
23
0
63
45
18

7.0     Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi Vijijini

Katika kutatua migogoro ya ardhi Halmashauri imefanikiwa kuandaa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 22 kati ya 63 vilivyopo katika wilaya ya Kiteto. Vijiji vyenye matumizi bora ya ardhi ni Ndaleta, Laalala, Mbigiri, Chapakazi, Kinua, Namelock, Kimana, Loltepes, Engusero Sidan, Emarti, Nhati, Taigo, Krashi, Ndiligish, Olkitikiti, Makame, Ndedo, Katikati, Ilkuishbor, Ngabolo Lerug na Ngapapa. Aidha mipango ya matumizi bora ya ardhi ya Vijiji vya Olpopong’, Partimbo, Ilera na Engongungare ipo katika hatua za mwisho kukamilishwa kupitia mikutano mikuu ya vijiji husika. Vijiji ambavyo havijaandaliwa matumizi bora ya ardhi ni Osteti, Engusero engine,  Njiapanda, Sunya, Asamatwa, Olgira, Mesera, Laiseri, Ndotoi, Magungu, Lengatei, Lesoit, Zambia, Kijungu, Njoro, Mwanya, Kiperesa, Mwitikira, Chekanao, Dosidosi, Nchinila, Chang’ombe (Dongo), Logoeti, Chang’ombe (Sunya), Loolera, Lembapuli, Amei, Chang’ombe (Njoro) na Ndorokoni.

8.0   MIGOGORO MBALIMBALI YA ARDHI WILAYANI KITETO KATIKA KIPINDI CHA NOVEMBA, 2015 HADI JANUARI, 2017

Halmashauri ya Kiteto ni miongoni mwa halmashauri zenye migogoro ya ardhi. Migogoro hii imegawanyika katika makundi matano (5) kama ifuatavyo;

Migogoro kati ya wakulima na wafugaji,

 Wananchi dhidi ya hifadhi za jamii mfano wa hifadhi ya Emboley Mutangos, hifadhi ya Makame WMA, Hifadhi ya Msitu wa SULEDO na maeneo ya hifadhi yaliyotengwa na vijiji.

 Migogoro ya kuvamia  mashamba makubwa yenye hati miliki,

Migogoro ya mipaka ya kijiji na kijiji,

Migogoro ya mipaka kati ya wilaya ya Kiteto na wilaya jirani.

8.1.0 HALI HALISI YA MIGOGORO YA ARDHI ILIYOPO

8.1.1 Migogoro kati ya wakulima na wafugaji 

Kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji ambayo hujitokeza mara kwa mara katika wilaya yetu. Maeneo yanayoathiriwa sana na migogoro hii ya wakulima na wafugaji iko katika vijiji vya Olpopong,  Ilera, Chekanao, Ndirigish, Mwitikira,  Kimana, Engusero Sidani, Kijungu, Mwanya, Ndaleta Kimana, Namelock, Kinua na Loltepes, Magungu na Emarti.

Sababu kubwa zinazosabisha migogoro hii ni kama ifuatavyo;

  • Maeneo mengi ya wilaya kutokuwa na mipango ya matumizi bora ya ardhi.
  • Wananchi kutoheshimu mipango ya matumizi bora ya ardhi katika maeneo yenye mipango ya matumizi waliyojiwekea.
  • Wananchi wengi kutofuata utaratibu wa kisheria kupata ardhi. Jambo hili husababisha wananchi wengi kuvamia maeneo yaliyokwishatengwa kwa matumizi mabalimbali.

8.1.2 Wananchi dhidi ya hifadhi za jamii.

Kumekuwa na uvamizi unaofanywa na wananchi kwenye hifadhi za Emboley Mutangos inayoundwa na vijiji 8 vya Kimana, Namelock, Loltepes, Nhati, Emarti, Engusero Sidan,Lerug na Ndirigish,  hifadhi ya Makame WMA inayoundwa na vijiji vya Makame, Ndedo, Ilkiushbor,Katikati na Ngabolo, Hifadhi ya Msitu wa SULEDO inayoundwa na vijiji vya Sunya, Lengatei, Mesera, Asamatwa, Olkitikiti, Engang’uengare, Loltepes, Laiseri, Olgira, Ndotoi. 

Uvamizi huu mara nyingi unafanywa na wananchi kutoka nje ya wilaya ya Kiteto ambao wanahitaji maeneo kwa ajili ya kilimo na mifugo.

 Sababu za uvamizi huu ni;

  • Wananchi kutafuta maeneo kwa ajili ya kilimo na malisho
  • Wananchi kutofuata utaratibu wa kisheria katika kupata ardhi ya kilimo ambapo kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi Na.5 ya mwaka 1999 Kifungu 51 -57 ambavyo vinaeleza utaratibu wa kila mwananchi kupata ardhi kijijini.
  • Mamlaka za vijiji wakati mwingine kuwahalalishia wananchi kukaa ndani ya hifadhi hizi, mfano Kijiji cha Ndotoi kimewahalalishia wananchi 33 jamii ya wafugaji waishi ndani ya hifadhi ya msitu wa SULEDO kinyume na sheria na makubaliano ya jumuia inayounda SULEDO.

8.1.3 Migogoro ya kuvamia mashamba makubwa yenye hati miliki, 

Kumekuwa na migogoro kati ya Kijiji na wananchi wenye mashamba makubwa ambayo husababishwa na shamba kuwa katika vijiji viwili wakati hapo awali shamba lilitolewa na kijiji kimoja. Mfano wa mgogoro huu ni Shamba Namba 559 linalomilikiwa na Benedict Kiroya Loosurutia lipo katika Vijiji vya Kimana na Namelock. Shamba hili nyaraka za umiliki kuonesha mmiliki amepewa ardhi kupitia kijiji cha Kimana. Kwa sasa kijiji cha Namelock kimegawa sehemu ya shamba inayoangukia katika kijiji hicho kwa watu wengine.Juhudi za pamoja za Ofisi ya Mkuu wa Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya,Uongozi wa Kijiji na mmiliki zimefanyika ili kubaini wale wote waliopewa ardhi katika shamba hilo bila kufuata sheria ili kuwaondoa.

Shamba lingine lenye malalamiko ni shamba lililopo katika Kijiji cha Emarti ambalo linamilikiwa na Dr. Charles Mazengo lina ukubwa wa ekari 547.27. Shamba hili nyaraka zinaonyesha alipewa na kijiji cha Magungu wakati kijiji cha Emarti kikiwa ni kitongoji cha Magungu. Kwa sasa wananchi wa Kijiji cha Emarti wanataka mmiliki huyu aondolewe kwenye shamba hilo.

8.1.4 Migogoro ya mipaka ya kijiji na kijiji, 

Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kumekuwa na migogoro ya mipaka kati ya Kijiji na Kijiji. Migogoro hii imeibuka katika kipindi cha kuanzia mwaka 2014 ambapo kulikuwa na wataalamu kutoka TAMISEMI, Wizara ya Fedha (Takwimu) na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambao walifanya mapitio ya mipaka ya vijiji na kupima upya mipaka hiyo. Katika upimaji huo baadhi ya vijiji mipaka yake imebadilika tofauti na ilivyokuwa hapo awali hivyo kusababisha malalamiko kutoka kwa wananchi. Vijiji vyenye mgogoro wa mipaka ni Kijungu na Lesoit na Lembapuli, Ngabolo na Ndaleta, Chekanao na Ilera, Nhati na Engusero Sidani na Ndotoi na Kimana na Ngabolo,Ndirigishi vs Namelock,Katikati vs Ndedo, Kijungu na Amei.

8.1.5 Migogoro mipaka kati ya wilaya ya Kiteto na wilaya jirani. 

Wilaya ya Kiteto inayo migogoro ya kimipaka baina yake na wilaya za jirani kama ifuatavyo;

  • Mgogoro baina ya Kiteto kwenye vijiji vinavyopakana na Simanjiro   (Makame na Ndedo) unaosababishwa na tafsiri isiyo sahihi kinyume na Tangazo la Serikali Na.113 la 1993 linalounda wilaya hizi.
  • Mgogoro baina ya Kiteto kwenye vijiji vinavyopakana na Kondoa (Ilkiushbour na Katikati). Mgogoro huu unasababishwa na tafsiri isiyo sahihi kinyume na Tangazo la Serikali Na. 65 la mwaka 1961 ambalo lilianzisha mikoa ya Arusha (Manyara) na Dodoma. Vilevile kuna tafsiri nyingine inayofanywa na wataalamu kwa kufuata Tangazo la Serikali Na. 185 ya tarehe 05.12.1980 ambalo limesababisha mgogoro ya mpaka huu.
  • Mgogoro baina ya Kiteto na Chemba ambao pia unasababishwa na tafsiri isiyo sahihi iliyofanywa na wataalamu wa timu ya uhakiki wa mipaka mwaka 2015 kinyume na Tangazo la Serikali Na. 65 la mwaka 1961 ambalo lilianzisha mikoa ya Arusha (Manyara) na Dodoma hususani kuutambua mlimahalisi wa Masagasi. Vilevile kuna tafsiri nyingine inayofanywa na wataalamu kwa kufuata Tangazo la Serikali Na. 185 ya tarehe 05.12.1980 ambalo limesababisha mgogoro ya mpaka huu.
  • Mgogoro baina ya Kiteto katika vijiji vinavyopakana na wilaya ya Kongwa  (Laiseri, Engusero Sidani,Dongo,Nhati,Emarti,Magungu,Olgine, Songambele, Dosidosi,Nchinila na Osteti). Mgogoro huu unasabishwa na tafsiri isiyo sahihi iliyofanywa na wataalamu wa timu ya uhakiki wa mipaka mwaka 2015 kinyume na Tangazo la Serikali Na. 65 la mwaka 1961 ambalo lilianzisha mikoa ya Arusha (Manyara) na Dodoma.
  • Mgogoro baina ya Kiteto na wilaya ya Kilindi katika vijiji vinavyopakana (Loolera, Lembapuli, Lesoit, Zambia, Lengatei, Mesera na Sunya). Mgogoro huu nao pia unasababishwa na tafsiri isiyo sahihi iliyofanywa na wataalamu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakati wa kazi ya kuongeza alama za kati hadi meta 500 kufuatia agizo la Mh.Wazri Mkuu Kassim Majaliwa alipotangaza kumalizika kwa mgogoro huu.kinyume na Tangazo la Serikali Na. 65 la mwaka 1961 ambalo lilianzisha mikoa ya Arusha (Manyara) na Tanga wataalam hao wamefanya tatizo hilo kubaki kama miaka ya mwanzo.

8.2 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA WILAYA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

Halmashauri kwa kushirikiana na Kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kiteto, pamoja na wananchi na wadau wengine wa maendeleo imefanya jitihada zifuatazo ili kutatua migogoro ya ardhi.

  • Halmashauri kwa kushirikiana Serikali Kuu pamoja na sekta binafsi imeweza kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 25 ambavyo ni Ndaleta, Laalala, Mbigiri, Chapakazi, Kinua, Namelock, Kimana, Loltepes, Engusero Sidan, Emarti, Nhati, Taigo, Krashi, Ndirigishi, Olkitikiti, Lerug,Engongungare, Partimbo na Ilera, Olpopong’ na Ngapapa, Makame, Ndedo, Katikati, Ilkiushbour na Ngabolo.
  • Halmashauri kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kiteto imeendelea kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kufuata utaratibu wa kisheria katika kupata ardhi ili kuondoa migogoro ya ardhi isiyokuwa ya lazima.
  • Wataalamu wa ardhi wameendelea kushirikiana na viongozi wa vijiji vyenye migogoro ya mipaka kubainisha mipaka ya vijiji hivyo. Pale panapotokea kutoelewana kuhusu mipaka hiyo wanashauriwa kukutanisha viongozi na wazee wa maeneo husika.
  •  Katika kutatua migogoro ya mipaka kati ya Kiteto na Wilaya za jirani, Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kiteto bado inaendelea kufanya vikao vya ujirani mwema na wilaya za jirani ili kutatua migogoro hii kwa kufuata maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ya kuzingatia Tangazo la Serikali Na.65 la mwaka 1961 na sio Tangazo la Serikali Na.185 la mwaka 1980.

8.3 CHANGAMOTO ZINAZOKABILI SEKTA YA ARDHI KITETO

8.3.1 Ufinyu wa bajeti katika sekta ya ardhi

Hii inasababisha malengo ya kiutendaji kutofikiwa katika sekta ya ardhi mfano ukosefu wa rasilimali fedha ya kutosha kunapunguza uzalishaji wa viwanja na mashamba yaliyopimwa tayari kumilikishwa.

8.3.2 Upungufu wa rasilimali watu na vitendea kazi

Sekta ya ardhi katika Wilaya ya Kiteto inaupungufu wa wataalamu wafuatao; Afisa Mipango miji na Vijiji, Mpima Ardhi na Maafisa Ardhi. Vilevile tuna upungufu wa vitendea kazi kama vile Hand held GPS, mafunzo kwa watumishi kuweza kutumia vifaa kufuatia teknolojia ya vifaa vya kazi vinavyotumika kwa sasa hususani katika upimaji ardhi na ukusanyaji maduhuli.

8.4.0 MATARAJIO YA BAADAE KATIKA SEKTA YA ARDHI

Matarajio ya Wilaya na Umma wa wanakiteto kwa siku zijazo ni haya yafuatayo;

  • Kupima kila kipande cha ardhi, kukimilikisha pamoja na kukisajili kwa mujibu wa sheria ili kupunguza migogoro ya ardhi na kumwezesha mwananchi kutumia ardhi kujiletea maendeleo.
  • Kuwa na mipango bora ya matumizi bora ya ardhi mjini na vijiji vyote 63 kwa lengo la kulinda mazingira, kuongeza tija, kuondosha migogoro kati ya wakulima na wafugaji na kuboresha miji yetu na makazi kwa ujumla.
  • Kutoa elimu kwa wananchi juu ya masuala mbalimbali ya ardhi ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo wa kushughulikia migogoro ya ardhi ndani ya vijiji vyetu na kata zetu ili kupunguza kushughulikia migogoro hiyo.
  • Kuboresha makusanyo ya maduhuli ya serikali yatokanayo na ardhi ili kuongeza pato la taifa na uwezo wa serikali katika kutoa huduma.
  • Kujenga ushirikiano wa karibu kati ya Halmashauri na sekta binafsi kwa lengo la kuongeza ubunifu, ubora na kasi ya huduma katika sekta hii na kupunguza kero zilizopo na zitakazojitokeza.

9.0 HIFADHI MBALIMBALI ZA JAMII WILAYANI KITETO.

9.1:     Hifadhi ya Mazingira - Emborley Murtangos.

 Hifadhi ya Mazingira ya Emborley Murtangos ilianzishwa kama Jumuiya ya Kijamii iliyojumuisha vijiji nane (8) vya Kimana, Lerug, Taigo, Kinua, Loltepes, Engusero Sidan, Ndirigish na Namelock.  Jumuiya hii ilikuwa na eneo lenye ukubwa wa hekta 133,333.15 yenye jumla ya wakaazi 9,640 kwa mujibu wa sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 ambapo lengo lake lilikuwa ni kuhifadhi Mazingira pamoja na shughuli nyingine za kiuchumi zitakazoamuliwa na vijiji vilivyounda Jumuiya hii.

Hifadhi hii ilianza kuvamiwa na wakulima tangu mwaka 2004 ambapo vijiji vikishirikiana na Halmashauri ya Wilaya viliendesha operesheni mara kwa mara hadi mwaka 2007 ambapo wakulima waliishtaki Halmashauri ya Wilaya katika Mahakama Kuu kitengo cha Ardhi Dar es Salaam. Kesi hii iliendeshwa kwa muda mrefu hadi kufikia mwaka 2011 ambapo Mahakama ya Rufaa ya Tanzania ilipotoa hukumu na kuipa Halmashauri haki ya kuwa ndiyo mmiliki halali wa eneo la Hifadhi. Mwezi Septemba 2012, Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi Dar es Salaam ilikaza hukumu nakumteua dalali na kumwamuru kuendesha operesheni ya kuvunja vibanda, nyumba na kuwahamisha watu wote katika eneo la Hifadhi.  Zoezi la kubomoa nyumba na vibanda lilianza tarehe 29/11/2012 na kukamilika tarehe 16/12/2012.

Mnamo mwezi Septemba, 2014 Timu ya kuhakiki mipaka iliwasili Wilayani Kiteto kwa ajili ya kuhakiki mipaka ya vijiji vyote, Hifadhi ya Mazingira ya Emborley Murtangos na mipaka ya Wilaya jinsi inavyopakana na Wilaya zingine. Baada ya kuhakikiwa upya Hifadhi ya Emborley Murtangos ilibaki na eneo lenye ukubwa wa hekta 75,463 na mzunguko wa km 168. Kupungua huko kwa ukubwa ulitokana na makubaliano yaliyofikiwa na vijiji vinavyounda hifadhi hiyo.

Watalamu kutoka Tume ya Taifa ya Matumizi bora ya Ardhi kwa kushirikiana na Wilaya ilifanya mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji kumi (10) ikiwemo vijiji vinavyounda Hifadhi ya Emborley Murtangos katika hatua ya kwanza hadi ya nne (1 – 4) ambapo hatua ya tano na sita (5 – 6) bado kukamilika kutokana na changamoto ya upatikanaji wa fedha.

Hivi sasa zipo changamoto za wakulima na wafugaji kutaka kurudi kulima na kulishia mifugo ndani ya hifadhi hususani kipindi hiki cha kilimo. Hata hivyo uongozi wa Wilaya na vijiji umekuwa ukichukua hatua za kuwaondoa wavamizi hawa ndani ya hifadhi.

 

Emborley Murtangos imekuwa ni sehemu ya vyanzo vya migogoro ya Wakulima na Wafugaji na usimamizi wake unaigharimu sana Halmashauri kiasi kikubwa cha mapato yake (uwezeshaji mafuta) ili kuwezesha mazoezi mbalimbali ya kuwaondoa wavamizi katika hifadhi. Kwa minajili hiyo Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya imepanga kuvikutanisha vijiji husika (vilivyo changia ardhi katika uundaji wa hifadhi hiyo) kupitia wawakilishi wao ili kupata maoni juu ya namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa eneo. Kwa kufanya hivyo, tunaamini kutasaidia kupata ufumbuzi wa kudumu juu ya migogoro itokanayo na Emborley Murtangos na hatimaye kuondoa gharama kubwa za usimamizi wa eneo hilo.

9.2:     Msitu wa SULEDO

Msitu huu unatambulika kwa jina la “SULEDO” ambalo ni ufupisho wa Kata tatu za Sunya, Lengatei na Dongo ambazo zilikuwa na vijiji tisa (9) na sasa vipo vijiji kumi na tatu (13)

Msitu huu umepakana na Kata ya Kijungu kwa upande wa Kaskazini, Mashariki umepakana na Wilaya ya Kilindi (Tanga) na Kusini umepakana na Wilaya ya Gairo (Morogoro). Kwa upande wa Kusini Magharibi umepakana na Wilaya ya Kongwa (Dodoma) na Kata ya Dongo na Namelock (Kiteto) kwa upande wa Magharibi.

Kwa mujibu wa ramani ya mipaka iliyochorwa Novemba, 1999 lilikuwa eneo lenye ukubwa wa hekta 167,416. Mwaka 1997 Halmashauri za vijiji tisa (9) vilivyokuwa vinaunda Msitu wa SULEDO vilikubaliana kwa pamoja kupitia Kamati zake za Mazingira za kila Kijiji kuunda Kamati ya Kanda ya SULEDO yenye wawakilishi watatu toka kila kijiji kwa ajili ya usimamizi wa pamoja wa msitu. Kamati hii iliandaa mpango shirikishi wa usimamizi wa msitu huu mwaka 2000.

Baada ya Ulinzi wa msitu kuonekana kuimarika ilionekana ni vyema kutambuliwa kwa msitu huu kuwa msitu wa jamii wa SULEDO.

Ombi hili lilitumwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Kiteto ambalo lilikubalika na kutamkwa rasmi katika kikao cha baraza la Madiwani cha tarehe 27/04/2000.

Ombi la pamoja la kusajili msitu huu katika ngazi ya Taifa lilitumwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kwa Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki na Kwa kufuata utaratibu ambapo msitu ulitangazwa rasmi kuwa msitu wa ardhi ya vijiji vya SULEDO mwaka 2007.

Msitu wa SULEDO umezungukwa na jamii zenye asili ya Wamasai, Wakamba, wanguu na Wakaguru. Jamii hizi zinajishughulisha na shughuli za Kilimo na Ufugaji. Shughuli za Ufugaji kwa kiasi fulani zinategemea msitu wa Hifadhi hasa wakati wa kiangazi ambapo sehemu kubwa ya eneo liltengwa kwa ajili ya malisho halina nyasi za kutosha kukidhi mahitaji halisi ya Mifugo.

Aidha jamii inaendelea kuutegemea msitu huu kwa mazao mbalimbali ya msitu yakiwemo mbao za kujengea na kutengenezea samani, kuni, maji, matunda, madawa ya asili, uyoga, nyasi za kuezekea nyumba, fito, asali, nta pamoja na kusaidia kuvuta mvua katika eneo hilo.

Changamoto zinazokabili msitu huu ni kama ifuatavyo;

  • Wananchi wa ndani ya wilaya ya Kiteto na wengine kutoka nje ya wilaya kuendelea kufyeka ndani ya msitu wa SULEDO kwa lengo la kufungua mashamba.
  • Mipaka ya mikoa ya Manyara, Tanga wilaya ya Kilindi na Morogoro wilaya ya Gairo kubadilika hivyo kumega eneo la msitu wa suledo kwa zaidi ya kilometa nne kwa upana.
  • Baadhi ya wanasiasa kuwashawishi wananchi kuharibu mazingira kwa kufyeka msitu kwa maslahi yao.

Jedwali Na. 7 Maeneo ya vijiji/msitu na idadi ya wamilikaji wakati msitu unaanzishwa.

NO
JINA LA KIJIJI
ENEO LA JUMLA (ha)
ENEO LA MSITU (ha)
IDADI YA WATU (2002)
IDADI YA KAYA 
(2002)
1.
Laiseri
50,010
32,699
2,926
585
2.
Olkitikiti
38,613.45
30,812
1,108
222
3.
Loltepes
52,050
26,741
3,747
749
4.
Mutura (Engang’ongare)
31,025.41
19,952
997
199
5.
Asamatwa
33,860
19,375
3,331
666
6.
Olgira
23,280
18,026
1,51
230
7.
Sunya
16,850
10,061
5,584
1,117
8.
Lesoit
15,560
5,348
1,567
313
9.
Lengatei
8,710
4,402
3,778
756

Jumla
267,958.86
167,416
12,162
4,837

Chanzo: Ofisi ya Mkurugenzi (W) Kiteto, 2018

 

9.2:1     Shughuli zinazoendelea katika Mradi wa Hifadhi ya Msitu wa Jamii

SULEDO

 Hifadhi imeweza kuanzisha na kusimamia miradi mbalimbali kwa ajili ya uendelevu wa Msitu na kuongeza kipato kwa jamii zinazoishi ndani ya Hifadhi. Ifuatayo ni orodha ya miradi iliyoanzishwa na mradi wa Hifadhi ya Msitu wa Jamii – SULEDO.

9.2.2:     Mradi wa Ufugaji Nyuki

Mradi huu ulianzishwa mwaka 2011 chini ya Ufadhili wa SIDA kupitia ALAT baada ya kufanya upembuzi yakinifu (feasibility study). Mradi huu unatekelezwa katika vijiji vyote vya SULEDO na ina jumla ya vikundi 17 na wanachama 711. Kuna jumla ya mizinga 805 ya kisasa na mizinga zaidi ya 1000 ya asili.Hata hivyo, vikundi vyote vimepatiwa mafunzo ya ufugaji bora wa asali, urinaji, uchujaji na ufungashaji wa asali na kupeleka katika masoko.

9.2.3:    Mradi wa Mkaa

Mchakato wa utumiaji wa mabaki ya miti wakati wa uvunaji wa magogo ulianza sambamba na utengenezaji wa mkaa katika msitu bila kuathiri usalama wa mazingira. Vikundi vilifanyiwa mafunzo na TATEDO juu ya mbinu bora za kutengeneza mkaa bila kuathiri mazingira. Hadi sasa SULEDO imefanikiwa kuuza mkaa kutoka msituni katika soko la ndani ya wilaya na nje (Dar es Salaam) na pia kusajili kituo (depot) cha kushushia na kuuzia mkaa na mbao huko Dar es Salaam.

9.2.4:    Mradi wa Sawmill

SULEDO kwa ufadhili wa SIDA walifanikiwa kununua mashine ya kupasulia mbao aina ya Woodmizer Lt 20 mwanzoni mwa mwaka 2015. Baada ya mashine hii kufika SULEDO yalifanyika mafunzo kazini kwa miezi miwili kwa ushirikiano kati ya SIDA na Chuo cha Viwanda vya Misitu Tanzania (FITI) kilichopo Moshi. Mashine hii ilisadia kupasua mbao kwa ajili ya matumizi mbalimbali kuanzia mwezi Aprili hadi Septemba 2015 ambapo mashine hii iliharibika. Taarifa ya kuharibika kwa mashine hii ilipelekwa ALAT ambao wao ndio wasimamizi wa mradi na kwa kuwa mashine ilikuwa na gurrantee SULEDO haikuweza kutengeneza.

Kutokana na mgogoro uliokuwepo kati ya ALAT na SIDA mkataba wa mradi ulivunjika hivyo SULEDO waliokuwa sehemu ya mradi kushindwa kuendelea na ufadhili ambao ulikuwa uishie July 2017. SULEDO iliendelea na mkakati wa kutengeneza mashine ili kuendelea na kazi na walipata ushauri wa kitaalamu kuwa mashine hii itumie mfumo wa umeme kwa kuweka mota na kuunganisha kwenye umeme.Mpaka sasa mashine ndogo aina ya Ding’dong ndiyo inayotumika kwa ajili ya kupasua mbao.

Mpaka sasa SULEDO kwa ushirikiano na Halmashauri ilitengeneza madawati 2235 za shule za msingi na sekondari na pia kazi ya kutengeneza madawati 150 ya shule ya Sekondari Lesoit inaendelea.

9.3:     Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori   - MAKAME (WMA) 

Jumuiya ya Hifadhi Wanyamapori Makame (WMA) ilianzishwa kwa mara ya kwanza na kusajiliwa kama Jumuiya ya Kijamii chini ya Sheria (SOCIETIES Ordinance 1954) yenye usajili SO. No. 14307 wa tarehe 18, Mei, 2006. Usajili ulifanywa kabla ya kutolewa kwa kanuni za hifadhi za Wanyamapori (WMA) ya mwaka 2005 ambapo ni marekebisho ya Kanuni za mwaka 2002 zilizoundwa kutokana na sheria ya kuhifadhi Wanyamapori Na. 12 ya mwaka 1974.

INDEMA SOCIETY ni jina la AA kwa maana ya mamlaka kamili ya jamii (Community Based Organization - CBO) iliyopewa eneo la vijiji mama vitatu vya Irkiushibor, Ndedo na Makame vilivyounda jumuiya hii na baadaye mwaka 2002 kijiji cha Irkiushibor kiligawanyika na kuzaliwa kijiji kipya cha Katikati ndani ya ardhi yake na pia kijiji cha Ndedo kiligawanyika na kuzaliwa kijiji kipya cha Ngabolo mwaka 2010 ndani ya ardhi yake.

 Eneo lote la Vijiji hivyo vinavyounda Makame WMA lina ukubwa wa kilometa za mraba 4,854.5 na wakazi wapatao 8,487 (sensa 2012). Kati ya km hizo za mraba, eneo lililotengwa kwa ajili ya hifadhi ya Wanyamapori ni kilometa za mraba 3,719 sawa na asilimia 76.6 ya eneo lote.

Hivi sasa WMA Makame (Wildlife Management Area) inaundwa na vijiji vitano (5) ambapo vijiji cha Ngabolo na Katikati kiliongezeka. Kwa Mkoa wa Manyara zipo WMA mbili (Burunge WMA na Makame WMA) na hifadhi ya Taifa ya Tarangire zikiwezesha kuhifadhi Wanyamapori na kulinda baionuai pamoja na njia za Wanyama.

Mwaka 2009 “Certificate of Authorization ilitolewa na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali Na. 385.Shughuli zilizotekelezwa na Jumuiya ya Wanyamapori Makame katika kipindi cha 2014/2015 na 2015/2016 ni kama zifuatazo:-

Doria mbailimbali zilifanyika kwa nyakati tofauti ya kuzuia na kupambana na wavamizi wa maeneo ya Jumuiya kwa shughuli zisizoruhusiwa katika eneo lote la jumuiya  kwa askari wa WMA (Village Game Scout – VGS), askari wa Mamalaka za Hifadhi hasa kanda ya kaskazini (KDU), vijiji wanachama na Halmahauri ya wilaya. Majangili wengi walikamatwa na VGS kwa kushirikiana askari wa Mamlaka za uhifadhi Kanda ya Kaskazini  (KDU- Arusha, Tarangire), Pia Gobore mgeuzo , Rifle , Smg, Shortgun  na Pistal  pamoja na  mishale, mitego ya wanyama na ndege zote zilipelekwa kituo chapolisi Kiteto na nyingine zilipelekwa  KDU –Arusha, na Babati kwa hatua za kisheria zaidi.

Jumla ya VGS 33 walishiriki mafunzo katika vyuo mbalimbali.

Jumuiya ilinunua pikipiki tatu (3) ambazo zinatumika kwa shughuli za ulinzi wa wanyamapori, kiutawala na shughuli mbalimbali zitakazopangwa kwa maendeleo ya Jumuiya.

Bunduki tatu (3) aina tofauti tofauti zilinunuliwa na taratibu za umilikishwaji silaha zinaendelea kukamilishwa ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa ili umlikishwaji itolewe kwa WMA.

Vijana 9 walisomeshwa na 12 wanaendelea na masomo katika ngazi mbalimbali za elimu kama vile Astashahada, Stashahada, Shahada katika vyuo mbalimbali nchini.

Makame WMA kwa kushirikiana na muungano wa WMA Tanzania (AAC) walifanya mchakato wa kutafuta wawekezaji na kufanikiwa kuwapata wawekezaji wawili waliosaini mikataba ya uwindaji wa kitalii na Makame WMA. Kampuni hizo ni Fereck Safaris Ltd kitalu Masai East Open Area na kampuni ya Masai Plate [Tz] Ltd kitalu cha Irkiushibor na kitalu cha Talamai hakijapata mwekezaji hadi sasa.

Makame WMA ilifanikiwa kuwa  na mradi wa uhifadhi wa mazingira kupitia shirika la  Carbon Tanzania  uliozinduliwa  na balozi  wa wa Marekani mwezi wa Februari, 2016.

Kila kijiji kilipewa Tsh 30,000,000/= sawa na 150,000,000 milioni  kwa vijiji (5) na sawa 50% ya mapato ya WMA kama mgao wa vijiji wanachama wa WMA na kutumika  kutekeleza miradi maendeleo kama ifuatavyo;

  1. Katikati;, Kujenga vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi katikati ,ujenzi wa  masijala ya kijiji na kujenga nyumba ya mwalimu (2:1) na  ujenzi umekamilika.
  2. Irkiushibor; Kumalizia nyumba kiporo ya walimu shule ya msingi Irkiushibor nyumba imekamilika, ujenzi wa bweni la wasichana jengo limekamilika.
  3. Makame; Kumalizia mradi wa josho, kunyonya vyoo (4) vilivyojaa vya shule ya msingi Makame na ujenzi wa bweni la wasichana shule ya msingi Makame ambapo jengo liko katika hatua ya ukamilishaji.
  4. Ndedo; Kujenga madarasa mawili ya shule ya msingi ambayo yapo kwenye hatua ya ukamilishaji. Aidha Vijiji vyote vilitumia sehemu ya fedha hizo katika ujenzi wa Maabara moja (1) katika sekondari ya Ndedo.
  5. Ngabolo; Kujenga ofisi ya kijiji ambapo ujenzi umekamilika, kujenga madarasa mawili ya shule ya msingi ambapo ujenzi uliishia kwenye lenta.

Changamoto kubwa ya hifadhi hii ya Makame W.M.A ni kuvamiwa na wakulima katika vijiji vya Katikati, Ngabolo na upande wa Kimana. Vilevile hifadhi hii inaathiriwa na mpaka kati ya Kiteto na Simanjiro, Kiteto na Kondoa.

Matangazo

  • TANGAZO NAFASI ZA KAZI July 23, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA UTENDAJI WA KIJlJI III August 26, 2021
  • TANGAZO LA KUKODISHA VIBANDA March 01, 2022
  • Tangazo kwa wanainchi wa Kiteto nafasi za ajira toka jeshi la uhamiaji January 02, 2022
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE KITENGO CHA AFYA KINGA KWA KIPINDI CHA ROBO YA KWANZA JULAI - SEPTEMBA 2022

    October 21, 2022
  • TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA LISHE KIPINDI CHA ROBO YA PILI (OCTOBA-DISEMBA 2021)

    January 24, 2022
  • Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto wakiwa wanapitia rejea ya mafunzo ya PLANREP iliyoboreshwa

    December 22, 2021
  • Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Mh.Mbaraka Al Haji Batenga akizungumza kwenye kikao cha maendeleo ya Wilaya (DCC)

    December 16, 2021
  • Angalia zote

Video za matukio ya kiofisi na kitaifa.

MWENGE MAKABIDHIANO MKOA WA MANYARA 2018
Video Zaidi

Kiunganishi cha Haraka

  • Kupata Hati ya Mshahara

Viunganishi vya Tovuti Nyingine

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • IKULU
  • MANYARA
  • NECTA
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Hesabu ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Kibaya-Kiteto

    Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto

    Simu ya Mezani: +255 027-2552099

    Simu ya kiganjani:

    Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa