KITENGO CHA TEKNOLOJIA,HABARI,MAWASILILIANO NA MAHUSIANO ( TEHAMA)
UTANGULIZI
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ni miongoni mwa halmashauri zinazotekeleza muundo mpya wa halmashauri za Wilaya ambao uliidhinishwa 08.07.2011 na Waziri Mkuu Mh Mizengo P Pinda. Kwa sasa kitengo kina watumishi 5 ambao ni Afisa Mahusiano/habari , Maafisa TEHAMA 3 na Opereta wa kompyuta mmoja. Toka kuanzishwa kwake hadi sasa kitengo hiki kimejitahidi kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kufanikisha lengo namba 9 la serikali ambalo ni kuimarisha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.
Jukumu kubwa la kitengo hiki ni kusimamia masuala yote ya habari na mawasiliano ya halmashauri halikadhalika kusimamia mifumo yote ya halmashauri. Kitengo hiki kimegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni:
• Habari na Mahusiano
• TEHAMA
Majukumu ya Kitengo
• Kuandaa miadi ya mkurugenzi kukutana na kuongea na vyombo mbalimbali vya habari
• Kutoa ufafanuzi kwa vyombo vya habari na jamii kwa masuala mbalimbali yanayohusiana na halmashauri kwa kufuata maelekezo ya mkurugenzi
• Kuandaa machapisho mbalimbali kwa ajili ya kuhabarisha jamii kuhusiana na masuala mbalimbali ya halmashauri (machapisho kama vile vipeperushi, jarida, )
• Kuandaa mkutano wa waandishi wa habari (Press Conference) baina ya mkurugenzi/mwenyekiti wa halmashauri na waandishi wa habari.
• Kuratibu na kusimamia waandishi wa habari katika shughuli mbalimbali za halmashauri kama vile baraza.
• Kuhakikisha halmashauri inasajili na kutumia barua pepe za serikali (Government Mailing System) kwa ajili ya kutuma na kupokea taarifa za kiserikali.
• Kusimamia mawasiliano ya ndani na nje ya ofisi (Internal and External Communication)
• Kusimamia Mifumo yote ya halmashauri,ifuatayo ni mifumo inayosimamiwa
• Mfumo wa Hcmis(Lawson)
• Mfumo wa Rasilimali Fedha (Epicor)
• Mfumo wa Prem
• Mfumo wa Mapato ( Lgrcis)
• Kusimamia Mashine za kieletroniki zinazokusanya Mapato(POS Machine)
Kusimamia Matengenezo yote ya vifaa vya TEHAMA kwa kuhakikisha vifaa vyote vipo katika hali nzuri
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa