Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ina jumla ya Idara (13) na Vitengo sita (6). KunaTarafa saba (7), Kata ishirini na tatu (23), Vijiji sitini na tatu (63) na Vitongoji miambili themanini na moja (281).
Kimsingi Idara ya Utumishi na Utawala katika kutekeleza majumu yake inazingatiamisingi ya utawala bora katika kutoa huduma bora kwa watumishi na jamii kwa ujumla.
Majukumu ya Idara
i. Kuandaa bajeti ya mishahara na ikama ya watumishi.
ii. Kutafsiri na kushughulikia miundo ya Utumishi.
iii. Kuajiri kwa kuomba vibali vya ajira Utumishi Makao Makuu.
iv. Kupandisha vyeo na kuthibitisha watumishi kazini.
v. Kusimamia na kushughulikia maadili na nidhamu za watumishi kwakuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo.
vi. Kusimamia na kuhakikisha vikao na mikutano yote ya kisheri na kikanuni Katangazi zote inafanyika.
vii. Kuandaa na kusimamia mpango wa mafunzo kwa watumishi wakiwa nje nandani ya vituo vya kazi.
viii. Kushughulikia mafunzo ya kuwajengea uwezo Watumishi, WaheshimiwaMadiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa.
ix. Kutathimini utendaji kazi wa watumishi.
x. Kushughulikia mambo ya itifaki kwa watumishi.
xi. Kufanya ukaguzi wa Payroll ya mishahara kwa kwa kushirikiana na wakuu waIdara kila mwezi na kutolea taarifa iwapo kutakuwa na mapungufu au usahihiwa payroll husika.
xii. Kuhakikisha watumishi wote ambao muda wao umefikia ukomo kwa sababumbali mbali wanaondolewa katika payroll kupitia Mfumo wa LAWSON.
xiii. Kuandaa Tange kwa kila robo ya mwaka na mwaka mzima.
xiv. Kutafsiri sheria, kanuni na nyaraka mbali mbali za Serikali katika utumishi waumma.
xv. Kutekeleza miongozo na mazoezi ya kitaifa yanayo tolewa.xvi. Kusimamia ulinzi na usalama wa mali zote za Halmashauri.
xvii. Kushughulikia haki na stahiki za watumishixviii. Kusimamia Mifumo ya usafiri wa magari ya Halmashauri.
xix. Kushirikiana na Taasisi zingine katika masuala mbalimbali ya kiutendaji.Uhakiki wa WatumishiKuanzia mwezi wa Machi 2016 Idara imetekeleza zoezi la uhakiki wa watumishi hewapamoja na uhakiki wa vyeti vya watumishi na sasa bado tunaendelea na zoezi la uhakikikila mwezi kabla ya kulipa mishahara.
Mafunzo
Pia Idara kwa kutumia fedha za LGDG kwa mwaka wa fedha 2016/2017 yametolewamafunzo kwa Waheshimiwa Madiwani kuhusu utawala bora, na Wakuu wa Idara naVitengo nao walipata mafunzo yanayohusu Usambazaji wa Miongozo ya Mfumo waUtekelezaji wa Fedha za Maendeleo Kwenye MSM (LGDG) iliyoboreshwa.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa