Utangulizi
Wilaya hii ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 16,685 ambalo ni sawa na asilimia 34.1% ya eneo lote la Mkoa wa Manyara. Wilaya ya Kiteto ipo kati ya Longitudo 36° 15’ hadi 37° 25’ Mashariki na Latitudo 40° 31 hadi 6º 03‘ Kusini.
Wilaya ya Kiteto inapakana na Wilaya ya Kondoa Mkoa wa Dodoma wakati Kaskazini inapatikana na Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara, kwa upande wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Kilindi iliyopo Mkoa wa Tanga, Kusini Mashariki inapakana na Wilaya ya Gairo ambayo ipo Mkoa wa Morogoro na Kusini Mashariki inapakana na Wilaya ya Kongwa na Chamwino ambayo zipo Mkoa wa Dodoma. Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ni kati ya Wilaya sita (6) zinazounda Mkoa wa Manyara. Ilizinduliwa mnamo Julai mosi 1974 ikiwa katika Mkoa wa Arusha na baadae kugawanywa mwaka 1993 na kuwa Wilaya mbili (2) yaani Kiteto na Kimanjaro ambapo Mkoa wa Manyara ulianza rasmi Julai 2002 baada ya kugawanywa kutoka Mkoa wa Arusha.
Hali ya hewa
Wilaya ya Kiteto ipo katika mwinuko wa kati ya meta 1000 hadi meta 1500 toka usawa wa bahari, kuna misimu miwili ya hali ya hewa kwa mwaka ambayo ni Masika na Kiangazi. Masika huwa kati ya mwezi Disemba hadi Mei na Kiangazi kati ya Juni hadi Novemba. Wilaya hupata Mvua za wastani wa kati ya mm 500 – mm 650 kwa mwaka.
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa