IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
MUUNDO WA IDARA
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika katika Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ni Idara ambayo inasimamia na kutekeleza shughuli zote za kilimo cha mazao, usalama wa chakula na maendeleo ya Ushirika katika Wilaya.
Ofisi za Idara ya Klimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja na Idara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Wilaya Kiteto, zilizopo katika Mji mdogo wa Kibaya.
|
Idara hii inaundwa na sehemu (section) 10 ili kuwezesha utekelezaji wa shughuli zote za kila siku. Sehemu hizo ni Ushirika na Masoko, Huduma za Ugani, Uzalishaji wa Mazao, Takwimu – Kilimo, Pembejeo za kilimo na Afya ya Mimea, Mipango na Matumizi bora ya Ardhi katika Kilimo, Kilimo cha Umwagiliaji, Kilimo cha Mboga mboga na Matunda, Zana na mashine za Kilimo na Lishe katika Kilimo.
IDADI YA WATUMISHI
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ina jumla ya Watumishi wa kudumu 63 kati yao Watumishi 16 ni Wanawake na 47 ni Wanaume kufikia mwezi Machi 2018.
Watumishi walioko kazini :
Wataalam wa Kilimo 59
Wataalam wa ushirika 03 (1 ni wa Tume ya Ushirika)
Katibu Muhtasi 00
Mhudumu 01
Upungufu wa Watumishi :
Idara ina upungufu wa Watumishi 39 kwa mchanganuo ufuatao
Wataalam wa Kilimo 36
Wataalam wa Ushirika 2
Katibu Muhutasi 1
MAJUKUMU YA MSINGI YA IDARA YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA
MAJUKUMU KATIKA SEHEMU YA USHIRIKA NA MASOKO
2. MAJUKUMU KATIKA SEHEMU YA HUDUMA ZA UGANI
4. MAJUKUMU KATIKA SEHEMU YA CHAKULA NA LISHE KATIKA KILIMO
5. MAJUKUMU KATIKA SEHEMU YA PEMBEJEO ZA KILIMO
6. MAJUKUMU KATIKA SEHEMU YA ZANA ZA KILIMO NA MITAMBO
8. MAJUKUMU YA SEHEMU YA UZALISHAJI WA MAZAO
9. MAJUKUMU YA SEHEMU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
10. MAJUKUMU YA SEHEMU YA TAKWIMU KILIMO
WADAU WA MAENDELEO YA KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA WILAYANI:
Serikali katika Wilaya ya Kiteto, inafanya kazi katika kuleta maendeleo ya Kilimo ikiwa sambamba na Taasisi za Kiserikali, Sekta Binafsi, Mashirika ya Kimataifa, Taasisi za Kidini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, na Taasisi nyingine. Wadau hawa hushiriki katika kutoa huduma za ugani kwa kusaidia uenezaji wa teknolojia mpya au zenye tija Wilayani, Kuandaa na kusaidia uanzishaji au ujenzi wa miundombinu ya Kilimo na kufanya utafiti wa teknolojia mbalimbali ndani ya Wilaya. Wadau hawa ni pamoja na:
SHUGHULI ZA KILIMO:
Wilaya ina eneo lenye ukubwa wa Hekta 382,000 zinazofaa kwa kilimo, na kati ya hizo, takriban hekta 208,000, ndizo zinazotumika katika shughuli za kilimo, Mazao ya aina mbili hulimwa hapa Wilayani ambayo ni mazao ya chakula na mazao ya biashara. Mazao makuu ya chakula yanayolimwa ni Mahindi, Mtama na Maharage. Mazao makuu ya biashara yanayolimwa ni Alizeti, Mbaazi na Ufuta. Kilimo katika Wilaya hii huendeshwa kwa takriban asilimia 99.9, kwa kutegemea mvua, hasa kutokana na uwepo wa kiwango kidogo cha vyanzo vya maji vya kudumu.
Kilimo cha mahindi kinachoendeshwa kimseto na zao la mbaazi, ni mojawapo ya mbinu za kilimo zinazofanywa na wakulima wengi kwa lengo la kuongeza tija kimapato katika eneo linalotumika katika uzalishaji.
|
Kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2012, asilimia 58 ya Wakazi wote wa Wilaya ya Kiteto hujishughulisha na kilimo, kama shughuli yao ya msingi kwa ajili ya kuzalisha chakula na kujiongezea kipato.
|
Alizeti zao la mafuta ambalo linategemewa kibiashara na wakulima wengi wa Wilaya ya Kiteto
Uwele, mojawapo ya zao la chakula linalozalishwa Wilayani Kiteto, lenye uwezo wa kufanya vizuri kiuzalishaji katika eneo la nyanda kame kama Wilaya hii.
|
Kilimo cha mtama, mojawapo ya mazao yanayostahimili ukame na kuzalishwa kwa ajili ya kukidhi mahitaji ya chakula na Wakulima wa Kiteto
|
Kiteto inapatikana katika eneo ambalo linajumuisha hali ya hewa na tabianchi zinazotofautiana katika baadhi ya maeneo, hivyo kutoa fursa ya kuendesha uzalishaji wa mazao anuwai (Crop Diversity) ndani ya Wilaya. Lakini, sehemu kubwa imo katika eneo lenye nyanda kame, hivyo matumizi ya teknolojia na mbinu mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo, pasipo kuathiri uzalishaji hutumika katika uzalishaji. Hii ni pamoja na matumizi ya mbinu na teknolojia za kilimo hifadhi na jembe-makucha la trekta au tindo/Ripa ya trekta (Ripper) kwa ajili ya kutindua udongo na kuvuna maji ya mvua mashambani.
Mbinu ya kutindua udongo kwa kutumia jembe–tindo/ripa linalokokotwa na trekta, kama mojawapo ya teknolojia inayotumika katika kuvunja jasi kwenye udongo na kuvuna maji ya mvua kupitia mbinu za kilimo hifadhi.
|
Uandaaji wa mashamba kwa ajili ya kufanikisha kilimo cha mazao katika Wilaya hii hutekelezwa kwa kutumia zana bora za kilimo, ambapo takriban 84% hutumia matrekta makubwa, matrekta madogo (Powertiller), pamoja na zana zinazokokotwa na Wanyamakazi. Hali hii huongeza tija katika uandaaji wa mashamba, na kupunguza ugumu wa kazi ya uandaaji.
Mkulima akiandaa shamba lake kwa kutumia trekta, ikiwa ndio njia kuu inayofanywa na Wakulima wa Kiteto katika kufanikisha shughuli zao za uzalishaji mashambani.
|
SHUGHULI ZA UMWAGILIAJI
Wilaya ya Kiteto, inaendesha kilimo cha umwagiliaji, hasa cha mazao ya mbogamboga katika maeneo mbalimbali kwa kutumia vyanzo vya maji vilivyopo. Wilaya ina takriban ekari 37.5 zinazotumika katika kuendeshea kilimo hiki. Mazao ya mbogamboga yanayozalishwa ni pamoja na Mboga za Majani, Nyanya, Vitunguu, Ngogwe/Nyanya Chungu, Bamia,n.k. Maeneo yote humwagiliwa kwa kutumia teknolojia ya umwagiliaji wa moja kwa moja (Surface Irrigation), ila kuna ekari 5 zilizoendelezwa kwa teknolojia ya matone (Drip Irrigation) katika kijiji cha Olgira
Kilimo cha umwagiliaji kwa kutumia tekinolojia ya matone katika Skimu ya Umwagiliaji Olgira
Changamoto kubwa ya kilimo cha umwagiliaji katika Wilaya hii ni ukosefu wa mito inayotiririsha maji mwaka mzima na hivyo kufanya kilimo hiki kuwa cha kubahatisha.
Maendeleo ya Kilimo katika sekta hii hutekelezwa kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wa mazao yenye virutubisho vingi (kama vile mbogamboga na matunda) ndani ya Wilaya ili kupambana na Athari zinazoikabili jamii kutokana na lishe, hasa utapiamlo. Jitihada hizi hulenga katika kutoa mbinu ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuwapatia chakula kinachoundwa na mlo kamili Wanajamii wote ili kulikabili tatizo la uwepo wa utapiamlo kwa takriban 0.6% ya Watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano, ndani ya Wilaya, hali inayotishia afya zao za kimwili na ubongo. Vilevile, Kilimo hiki ni chenye uhakika, hivyo kuchangia katika kuimarisha hali ya usalama wa chakula ngazi ya Kaya na kipato; hivyo kufanikisha vita dhidi ya Maadui Ujinga, Maradhi na Umasikini.
MAFANIKIO YA SEKTA YA KILIMO
SHUGHULI ZA USHIRIKA:
Moja ya majukumu ya Idara ni kusimamia na kuendeleza shughuli za Ushirika, Wilaya ina Vyama vya Ushirika 41 vinavyojishughulisha na kuwaunganisha Wakulima/Wafugaji katika makundi yenye malengo ya kimaendeleo katika kuinua hali zao za kiuzalishaji, kujipatia mitaji ya kuwekeza katika shughuli zao za kiuchumi na masoko ya mazao yao. Kati ya hivyo, vipo Vyama vya ushirika vya masoko ya Kilimo (AMCOS) 16, vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS) 23 na Ushirika wa Viwanda (Industrial Cooperatives) 2 na chama cha Ushirika wa Maziwa (DairyCooperative Society) 1.
Kiwanda kidogo cha Ushirika wa Wazalishaji wa maziwa Kibaya (KDC), kilichopo katika Mji mdogo wa Kibaya
|
TAKWIMU ZA VYAMA VYA USHIRIKA HADI APRIL, 2018
AINA YA CHAMA
|
IDADI YA WANACHAMA |
||||
ME
|
KE
|
VIKUNDI
|
TAASISI
|
JUMLA
|
|
AMCOS
|
817
|
495
|
0
|
0
|
1312
|
SACCOS
|
895
|
670
|
39
|
0
|
1604
|
LIVESTOCK COOPERATIVE
|
22
|
39
|
0
|
0
|
61
|
DAIRY COOPERATIVE
|
12
|
23
|
0
|
0
|
35
|
INDUSTRIAL COOPERATIVE
|
2
|
28
|
0
|
0
|
30
|
JUMLA
|
1748
|
1255
|
39
|
0
|
3042
|
Kibaya-Kiteto
Anwani ya Posta: P.o.Box 98, Kibaya-Kiteto
Simu ya Mezani: +255 027-2552099
Simu ya kiganjani:
Barua Pepe: ded@kitetodc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halimashauri ya Kiteto.Haki zote zimehifadhiwa